Pata taarifa kuu
GAMBIA-HAKI

Gambia yatoa wito kwa wanawake waliofanyiwa ukatili kutoa ushahidi dhidi ya Jammeh

Aliye kuwa rais wa Gambia Yaya Jammeh, katika mkutano wa kilele cha ECOWAS, Machi 28, 2014.
Aliye kuwa rais wa Gambia Yaya Jammeh, katika mkutano wa kilele cha ECOWAS, Machi 28, 2014. ISSOUF SANOGO / AFP

Serikali ya Gambia inatoa wito kwa wanawake na wasichana nchini humo ambao walinyanyaswa kimapenzi na rais wa zamani Yaya Jammeh, kujitokeza na kutoa taarifa.

Matangazo ya kibiashara

Wito huu unakuja, baada ya mneguaji wa video Fatou Jallow, kudai kuwa alibakwa na Jammeh wakati alipokuwa rais mwaka 2015.

Ushahidi wake ni miongoni mwa ripoti ya shirika la haki za kibinadamu la Human Rights Watch ambayo inaelezea madai mengine ya ubakaji na unyanyasaji wa kingono uliotekelezwa na bwana Jammeh alipokuwa madarakani.

Fatou Jallow alibani kwamba yuko tayari kutoa ushahidi mbele ya tume ya haki na maridhiano nchini Gambia TTR ambayo imebuniwa na rais Adama Barrow ambaye alishinda uchaguzi wa mwezi Disemba 2016.

Tume hiyo ya haki na maridhiano inachunguza ukiukaji wa haki za kibinaadamu wakati wa utawala wa miaka 22 wa bwana Jammeh , ikiwemo ripoti za mauaji ya kiholela , ukatili na kukamatwa na kuzuiliwa kiholela.

Chama cha kiongozi huyo wa zamani cha APRC kimekanusha madai hayo.

Yaya Jammeh alilazimishwa kuondoka madarakani mwaka 2017 na kukimbilia nchini Equatorial Guinea.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.