Pata taarifa kuu
DRC-UPINZANI-FAYULU

Polisi wazuia maandamano ya upinzani jijini Kinshasa, mmoja apoteza maisha Goma

Polisi wakipambana na waandamanaji wa upinzani jijini Kinshasa
Polisi wakipambana na waandamanaji wa upinzani jijini Kinshasa Radio Okapi/Ph. John Bompengo.
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 2

Polisi jijini Kinshasa nchini DRC, wametumia mabomu ya kutoa machozi, kuwasambaratisha wafuasi wa upinzani waliokuwa wanaandamana wakiongozwa na aliyekuwa mgombea urais Martin Fayulu, huku mtu mmoja akiuawa kwa kupigwa risasi na polisi mjini Goma.

Matangazo ya kibiashara

Gari la Fayulu lilizuiwa na maafisa wa polisi, sawa na mwanasiasa mwingine wa upinzani, Waziri Mkuu wa zamani Adolphe Muzito.

Ripoti zinasema kuwa, polisi zaidi ya 50, walimzingira, Fayulu katika katika barabara ya Boulevard Lumumba na wakaamua kushuka kuzungumza na mkuu wa jeshi la polisi katika jiji hilo Sylvano Kasongo .

Maandamano ya leio, yalliitishwa na Fayulu na Jean Piere Bemba ambaye pia aliwasili nchini humo hivi karibuni akitokea nchini Ubelgiji, kwa kile walichosema ni kuendelea kupinga usindi wa rais Felix Tshisekedi wakati wa uchaguzi Mkuu uliofanyika mwezi Desemba mwaka 2018.

Akihojiwa na Televisheni ya France 24, rais Felix Tshisekedi alisema anaunga mkono hatua ya polisi kuzuiwa maandamano hayo, kwa hofu ya machafuko huku akieleza kuwa  kuna watu ambao hawaelewi maana ya demokrasia na uongozi usiotii sheria.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.