SUDANI-SIASA-USALAMA

Sudan: Baraza la Jeshi la Mpito latilia shaka makubaliano yaliosainiwa

Luteni Jenerali Mohamed Hamdan Dagalo, mkuu wa Baraza la kijeshi, Aprag Juni 22, 2019.
Luteni Jenerali Mohamed Hamdan Dagalo, mkuu wa Baraza la kijeshi, Aprag Juni 22, 2019. REUTERS/Umit Bektas

Baraza la kijeshi la mpito nchini Sudan linaendelea kutilia shaka pointi kadhaa za mikataba ambayo tayari iliyosainiwa na linataka mazungumzo yaanzishwe upya.

Matangazo ya kibiashara

Bara hilo limeomba kuchukuwa nafasi ya uongozi wa nchi katika serikali itakayoundwa.

Kauli hiyo inakuja siku mbili baada ya baraza hilo la kijeshi kutangaza siku ya Jumapili kuwa limejibu timu ya mseto ya usuluhishi (Umoja wa Afrika na Ethiopia) kwamba limeridhika na hoja ya timu ya usuluhishi.

Kwa mujibu wa makubaliano na mpango wa pamoja, Halmashauri Kuu ya uongozi wa nchi inatakiwa kuwa na wajumbe 15, raia 7 wa upinzani, askari 7 na mwanasia asioegemea upande wowote.

Siku ya Jumapili watu saba waliuawa katika makabiliano kati ya jeshi na waandamanaji.

Watu zaidi ya 200 walijeruhiwa katika makabiliano hayo. Maelfu ya watu waliandamana kote nchini wakiomba jeshi kukabidhi madaraka kwa raia.