DRC-WFP-NJAA-UTAPIAMLO-AFYA

Shirika la Mpango wa Chakula Duniani: Tuna wasiwasi ya njaa kuzuka Ituri

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, wakaazi wa baadhi ya maeneo ya Ituri wanakabiliwa na uhaba wa chakula.
Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, wakaazi wa baadhi ya maeneo ya Ituri wanakabiliwa na uhaba wa chakula. © SAMIR TOUNSI / AFP

Visa vya utapiamlo vinaripotiwa katika mkoa wa Ituri, unaoendelea kukumbwa na machafuko hasa ya kikabila, kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP).

Matangazo ya kibiashara

Tayari watu 160 wameuawa katika machafuko hayo tangu mwezi Aprili na watu 300,000 wameyahama makazi yao.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambayo ina wakaazi milioni 13 wanaokabiliwa na uhaba wa chakula, inakabiliwa na mlipuko wa pili mbaya wa njaa duniani baada ya Yemen.

Umoja wa Mataifa umetoa wito wa kusaidia ili maafa zaidi yasiwezi kutokea .

"Je, tunaweza kusema leo kwamba watu wanakabiliwa na njaa katika mkoa wa Ituri? "Jibu ni ndiyo", WFP limesem akatika taarifa yake.

Hervé Verhoosel, msemaji wa Shirika la Mpango wa Chakula cha Dunia (WFP), amethibitisha taarifa hiyo ya shirika la Umoja wa Mataifa.

Takwimu bado hazijulikani kujua ni watu wangapi ambao wamefariki kwa njaa katika mkoa wa Ituri. Uhakika pekee ni kwamba kwa sababu ya machafuko ya hivi karibuni, njaa imeanza kusababisho vifo katika baadhi ya maeneo katika mkoa huo.

"Tunataka kuongeza msaada mara tatu, amesema Hervé Verhoosel, hasa katika mkoa huu na walengwa hasa ni watu wakimbizi wa ndani, yaani watu waliotoroka makaazi yao na kukimbilia katika maeneo salama. Wakimbizi ni wengi kwa sababu ya machafuko ya kikabila kwa sasa. Kwa hiyo, tutaongeza mara tatu kutoka 116,000 hadi 300,000 au juu zaidi. Hili nijambo ambalo tayari tumeanza kulishughulikia kwa sasa. Hata kama bado hatujapata fedha zote. Na ni kweli kwamba tunatafuta fedha, " ameseongeza Verhoosel.

WFP bado inatafuta dola milioni 155 ili kutekeleza shughuli zake nchini DRC hadi mwishoni mwa mwaka huu. Dola milioni 35 zimetengwa katika mapambano dhidi ya maambukizi ya virusi vya Ebola, ugonjwa ambao umeathiri sana mkoa wa Ituri, ikiwa ni mkoa wa pili kuathirika na ugonjwa huo baada ya mkoa wa Kivu Kaskazini.