LIBYA-IOM-WAHAMIAJI-USALAMA

Libya: Wahamiaji 300 waendelea kuzuiliwa Tajoura

Kituo wanakozuiliwa wahamiaji cha Tajoura kiliteketezwa kwa shambulio la anga Julai 2, 2019.
Kituo wanakozuiliwa wahamiaji cha Tajoura kiliteketezwa kwa shambulio la anga Julai 2, 2019. MAHMUD TURKIA / AFP

Wahamiaji 300 bado wanazuiliwa katika kituo cha wahamiaji cha Tajoura, kilicho shambuliwa mapema wiki hii nchini Libya na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 44.

Matangazo ya kibiashara

Katika shambulio hilo la anga watu 130 walijeuhiwa kwa mujibu wa ofisi ya shirika la umoja wa Mataifa la wahamiaji (IOM).

Kati ya wahamiaji zaidi ya 600 ambao walikuwa katika kituo cha Tajoura, "300 bado wanazuiliwa," na wananufaika na msaada wa kibinadamu kutoka shirika la IOM, afisa anayehusika na mawasiliano kwenye shirika hilo, Safa Msehli, ameliambia shirika la Habari la AFP.

Bi Msehli hakuweza kuthibitisha ripoti ambazo zinasema kuwa wahamiaji kadhaa walitoroka siku ya Jumanne usiku baada ya shambulio la angani.

Katika taarifa, shirika la IOM, hata hivyo, limesema leo Alhamisi kuwa timu zake zimewaona na kuwapeleka hospitali kundi la wahamiaji waliojeruhiwa katika maeneo jirani, baada" kutoroka mji wa TAjoura kufuatia shambulio hilo.

"Shambulio la Jumanne usiku liligharimu maisha ya watu wasiokuwa na hatia, na pande zote zinapaswa kuchukua hatua mara moja," amesema kiongozi wa ujumbe wa IOM nchini Libyan, Othman Belbeisi, akinukuliwa na taarifa hiyo.

"Maumivu ya wahamiaji nchini Libya yameshindwa kuvumiliwa, lazima iwe wazi kuwa Libya haiwezi kuwa salama na kwamba maelfu ya watu bado wako hatari," ameongeza.