AU-BIASHARA-UCHUMI

Mkataba wa kibiashara kati ya mataifa ya Afrika kuanza rasmi kutumika Julai 1, 2020

Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika, Moussa Faki Mahamat, katika Mkutano wa Umoja wa Afrika, Niamey, Niger, Julai 7, 2019.
Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika, Moussa Faki Mahamat, katika Mkutano wa Umoja wa Afrika, Niamey, Niger, Julai 7, 2019. REUTERS© REUTERS/Tagaza Djibo

Nchi 54 za bara la Afrika ispokuwa Eritrea zimetia saini mkataba wa kibiashara kati ya nchi hizo (Zlec) au (Zlecaf). Mkataba ambao utaanza kutumika rasmi Julai 1, 2020, kwa mujibu wa taarifa ya Umoja wa Afrika.

Matangazo ya kibiashara

Zaidi ya viongozi 32 walishiriki mkutano huo uliofanyika katika mji mkuu wa Niger, Niamey.

Mji mkuu wa Ghana, Accra, ndio umechaguliwa kuwa makao makuu ya sekretarieti ya jumuiya hiyo.

Viongozi wengi walioshiriki mkutano huo wamesema hatua ya kuanzisha soko hilo la pamoja inaleta hitoria mpya barani Afrika.

Jumuiya hii ya Biashara huria barani Afrika ambayo tunazindua leo ni mojawapo ya miradi muhimu ya ajenda ya Afrika. Kwa hiyo Afriak imekamilisha ndoto yake amesema Moussa Faki Mahamat, Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika.

Makubaliano hayo yamefikiwa baada ya miaka 17 ya mashauriano makali na ambayo yaliafikiwa rasmi mwishoni mwa mwezi Aprili mwaka huu wakati makubaliano hayo yalipovuka kiwango cha uzinduzi kilichohitaji kuratibishwa na angalau mataifa 22.

Nigeria, taifa lenye idadi kubwa zaidi ya watu na uchumi mkubwa zaidi barani Afrika, ilitangaza wiki hii kwamba itajiunga na makubaliano hayo ya Niamey baada ya kujiondoa bila kutarajiwa mwaka uliopita.