ALGERIA-MAANDAMANO-SIASA-UCHAGUZI

Algeria: Mkuu wa majeshi aendelea kuonyesha uungwaji wake mkono kwa rais wa mpito

Ahmed Gaid Salah Aprili 2, 2019 Algiers.
Ahmed Gaid Salah Aprili 2, 2019 Algiers. © Canal Algerie /Handout via Reuters

Mkuu wa majeshi nchini Algeria Ahmed Gaid Salah amezungumzia kuhusu hali ya kisiasa nchini humo kwa sasa, akisema kuwa anaendelea kumuunga mkono rais wa mpito Abdelkader Bensalah, ambaye muda wake wa kuhudumu kama rais umemalizika rasmi Jumanne wiki hii.

Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo amebaini kwamba jeshi bado linakubaliana na hoja ya kufanyika uchaguzi haraka iwezekanavyo. Lakini pia katika hotuba yake amewaonya waandamanaji.

"Wale ambao hawaungi mkono jeshi ni maadui". Huo ni ujumbe wa Mkuu wa majeshi ya Algeria akiwaonya waandamanaji, hasa wale wanaoendelea kudai kuwepo na utawala wa kiraia na sio wa kijeshi na kwa wale ambao wamekuwa wakiendelea kubebelea bendera zilizopigwa marufu nchini humo, lakini pia kwa wale wanaowaunga mkono na kustumu kuzuiliwa kwa wafungwa wa maoni au wa kisiasa.

Kwa upande wa Ahmed Gaïd Salah amesema, watu hawo wote wanachangia kuleta vurugu nchini na kuchangia kuongezeka kwa vitendo vya rushwa, huku akionya: jeshi lina jukumu la kuweka nchi sawa na kukomesh rushwa. Ameiomba mahakama kutumia sheria ya kukabiliana na hali hiyo.

Tangu kujiuzulu kwa Abdelaziz Bouteflika, viongozi wa kisiasa zaidi ya ishirini wamewekwa kizuizini. Zaidi ya watu sitini pia wanakabiliwa na mkono wa sheria, baada ya kukamatwa katika maandamano wakibebelea bendera zilizopigwa marufuku.