AFRIKA-UGAIDI-AU-UN-USALAMA

G5 Sahel: Guterres na Faki Mahamat waomba Baraza la Usalama kuungwa mkono

Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika, Moussa Faki Mahamat.
Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika, Moussa Faki Mahamat. © Flickr/CC/Chatham House/©Suzanne Plunkett 2017

Maafisa 1,130 kutoka nchi 185 wanashiriki tangu Jumatano hadi Alhamisi wiki hii mkutano wa kukabiliana na ugaidi na kuzuia msimamo mkali unaoweza kuhatarisha usalama wa nchi barani Afrika.

Matangazo ya kibiashara

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres na Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika, Moussa Faki Mahamat, wametumia fursa katika mkutano huo kuomba msaada kwa kikosi cha G5 Sahel, chenye askari 5,000 kutoka Mauritania, Mali, Burkina faso, Nigeria na Chad waliotumwa kupambana dhidi ya ugaidi katika eneo hilo.

Miaka mitano tayari imekamilika tangu kikosi cha G5 kuanzishwa. Hata hivyo, jitihada bado zinaendelea japokuwa vita dhidi ya magaidi si rahisi. Jumatano wiki hii, Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika, Moussa Faki Mahamat, alinyooshea kidole Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. "Ninakubali kwamba tumeshindwa kuelewa kwa nini wamechelewa kufadhili shughuli za kuimarisha usalama barani Afrika. Nchi za Kiafrika zimetoa uwezo wao mdogo kwa kuitikia zoezi la kukabiliana na tishio hilo kubwa na ombi kutoka Afrika halijaweza kupata mpaka sasa msaada kutoka Umoja wa Mataifa ili kukabiliana na tishio hilo, na ni wajibu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa."

Kikosi cha G5 Sahel hakikuwekwa kwenye vipengelea vya mkataba wa Umoja wa Mataifa. Kwa hiyo haiwezekani kutumia uwezo wa Umoja wa Mataifa au kubadilisha kikosi hicho kuwa walinda amani wa Umoja wa Mataifa.

Wakati huo huo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema kwa masikitiko makubwa kuwa kikosi hicho kinajitaji msaada kutoka Umoja wa Mataifa. "Niliiambia wazi Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwamba kikosi cha G5 Sahel kinapaswa kufadhiliwa na michango ya Umoja wa Mataifa, na hivyo kikosi hicho kuwa na nguvu zaidi. Hoja yangu haikukubaliwa. Kwa bahati mbaya ugaidi unaendelea. Sasa Ghana, Benin, Togo, Cote d'Ivoire wanasema ugaidi unakaribia kwenye mipaka yao. Ni muhimu kwamba vikosi vya kupambana na kigaidi vya Afrika kuwa na mamlaka kamili, " Antonio Guterres amsema.