LIBYA-UFARANSA-USALAMA-USHIRIKIANO

Makombora ya jeshi la Ufaransa Libya:Tripoli yaomba Paris kutoa ufafanuzi haraka

Moja ya kombora aina ya Javelin yaliyogunduliwa na wapiganaji wa serikali ya umoja wa kitaifa ya Libyan (GNA) Gharyan, Magharibi mwa Libya, Juni 29, 2019.
Moja ya kombora aina ya Javelin yaliyogunduliwa na wapiganaji wa serikali ya umoja wa kitaifa ya Libyan (GNA) Gharyan, Magharibi mwa Libya, Juni 29, 2019. AFP

Serikali ya umoja wa kitaifa nchini Libya (GNA), inayotambuliwa na Umoja wa Mataifa, imeiomba Ufaransa kutoa ufafanuzi "haraka", baada ya Ufaransa kutambua kuwa makombora yaliyogunduliwa katika ngome kuu ya majeshi ya Marshal Khalifa Haftar karibu na mji wa Tripoli ni mali yake.

Matangazo ya kibiashara

Katika barua yake, Waziri wa Mambo ya Nje wa serikali ya umoja wa kitaifa nchini Libya, Mohamad Tahar Siala, amemuomba mwenzake wa Ufaransa, Jean-Yves Le Drian, "kutoa ufafanuzi wa haraka kuhusu jinsi gani silaha za Ufaransa zilizogundua huko Gharyan zilifikia majeshi ya Haftar, ni wakati gani zilipelekwa na jinsi gani? ", Kulingana na taarifa kutoka kwa Wizara ya Mambo ya Nje.

Bw Siala pia ametaka kujua "idadi ya silaha" ambazo Ufaransa ulituma kwa Marshal Haftar, na "ambapo kuwepo (nchini Libya) inapingana na taarifa ya serikali ya Ufaransa (...) kuunga mkono serikali ya umoja wa kitaifa ya Libya (GNA), kama serikali inayotambuliwa kimataifa ".

Siku ya Jumatano Ufaransa ilikiri kwamba makombora yaliyogunduliwa katika kambi ya majeshi ya Marshal Haftar karibu na Tripoli yalikuwa yake, huku ikikanusha kwamba haijampa slaha za aina yoyote Jenerali Haftar.

"Makombora aina ya Javelin yaliyogunduliwa huko Gharyan, kweli ni mali ya jeshi la Ufaransa, ambayo iliyanunua chini Marekani," Wizara ya Ulinzi ya Ufaransa ilisema siku ya Jumatano.

"Makombora hayo yalitumwa kwa aili ya ulinzi wa kikosi cha maafisa wa Ufaransa kwa lengo la upelelezi katika masuala ya kupambana dhidi ya ugaidi, wizara ya majeshi imebaini, na kuthibitisha kwamba Ufaransa ina askari wake nchini Libya.