SUDANI-SIASA-USALAMA

Sudan: Serikali ya kijeshi yazima jaribio la mapinduzi

Jenerali Jamal Omar, mjumbe wa Baraza la keshi la Mpito, Julai 4, 2019.
Jenerali Jamal Omar, mjumbe wa Baraza la keshi la Mpito, Julai 4, 2019. © ASHRAF SHAZLY / AFP

Mwakilishi wa utawala wa kijeshi nchini Sudan Jenerali Jamal Omar amethibitisha kwenye televisheni ya taifa kwamba jeshi limefaulu kuzima jaribio la mapinduzi.

Matangazo ya kibiashara

Tangazo hili linakuja wakati utawala wa jeshi na wanasiasa wa upinzani wanatarajia kutia saini mkataba wa mwisho wa kugawana madaraka uliofikiwa chini ya mwamvuli wa Umoja wa Afrika na Ethiopia.

"Maofisa wa jeshi na askari, pamoja na maafisa wa idara ya ujasusi, ikiwa ni pamoja na baadhi waliotaafu ni miongoni mwa watuhumiwa wa jaribio hlo la mapinduzi, " amesem Jenerali Jamal Omar.

Ambebaini kwamba maafisa 12 na askari wanne wamekamatwa, ili kubaini waliohusika na jaribio hilo lililotibuliwa, ambalo hakutaka kutaja ikiwa lilifanyika wakati gani.

Kwa mujibu wa Jenerali Jamal Omar, lengo lilikuwa kupinga mkataba wa kugawana madaraka uliofikiwa wiki iliyopita kati ya utawala wa kijeshi na upinzani. Mkataba ambao nakala yake ya mwisho iliwasilishwa jana usiku kwa wajumbe wawili. Na unatarajiwa kutiliwa saini katika siku zijazo.

Kuna mgawanyiko katika vikosi vya usalama na ulinzi kwa sasa. Aidha, mwezi uliopita, Baraza la kijeshi la Mpito lilisema kulikuepo na mpango wa jaribio la mapinduzi na kulazimika kuwakamata baadhi ya watu.