SUDANI-SIASA-HAKI

Sudan yaombwa kumuachilia huru mwanahabari Michael Christopher

Waandamanaji wakibebelea bango lenye picha ya kiongozi wa Baraza la Kijeshi la Mpito Abdel fattah al-Burhan , Mei 31, 2019.
Waandamanaji wakibebelea bango lenye picha ya kiongozi wa Baraza la Kijeshi la Mpito Abdel fattah al-Burhan , Mei 31, 2019. ASHRAF SHAZLY / AFP

Mke wa Mwanahabari maarufu nchini Sudan Kusini Michael Christopher, anaomba maafisa wa usalama kumwachilia huru mume wake au kumfungulia mashtaka Mahakamani.

Matangazo ya kibiashara

Christopher ambaye ni Mhariri wa Gazeti la Kiarabu la Al Watan, amekuwa akizuiwa na maafisa wa usalama tangu wiki iliyopita.

Alikamatwa wakati akisafiri kwenda jijini Nairobi, nchini Kenya, kupata matibabu na pasi yake ya kusafiria kuchukuliwa.

Marekani na mashirika ya kimataifa ya kutetea haki za binadamu, pia yanataka aachiliwe huru.