UFARANSA-COMORO-USHIRIKIANO

Ufaransa na Comoro watafautiana kuhusu mmiliki halisi wa Kisiwa cha Mayotte

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na mwenzake wa Comoro Azali Assoumani, Julai 22, 2019, Elysée.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na mwenzake wa Comoro Azali Assoumani, Julai 22, 2019, Elysée. Ian Langsdon/Pool via REUTERS

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amekuwa na mazungumzo na mgeni wake rais wa Comoro Azali Assumani, ambapo wawili hao wameonekana kutofautiana kuhusu swala la kisiwa cha Mayotte.

Matangazo ya kibiashara

Mbele ya vyombo vya habari rais Macron alisisitiza kuwa Mayotte ipo upande wa Ufaransa, kauli ambayo ameitoa kutokana na kumbukumbu ya kura ya maoni ya wananchi wa Mayotte kuamuwa kuwa wafaransa.

Hata hivyo licha ya wananchi wa Mayotte kupiga kura mara kadhaa kubaki upande wa Ufaransa, rais wa sasa Azali Asumani amepinga hatua hiyo na kueleza kwamba Mayotte ni Comoro.

Licha ya kutofautiana kuhusu swala la Mayotte, viongozi hao wamekubaliana kuendelea kushirikiana kwa faida ya pande zote mbili.