SOMALIA-AL SHABAB-USALAMA

Sita wauawa katika shambulio dhidi ya ofisi ya meya Mogadishu

Mwakilishi Maalum mpya wa Umoja wa Mataifa nchini Somali, James Swan (kushoto), akipokelewa na Meya wa Mogadishu (kulia) muda mfupi kabla ya shambulio la dhidi ya ofisi ya Meya, Julai 24, 2019. Meya wamji muu wa Somalia Abdirahman Omar Osman amejeruhiwa.
Mwakilishi Maalum mpya wa Umoja wa Mataifa nchini Somali, James Swan (kushoto), akipokelewa na Meya wa Mogadishu (kulia) muda mfupi kabla ya shambulio la dhidi ya ofisi ya Meya, Julai 24, 2019. Meya wamji muu wa Somalia Abdirahman Omar Osman amejeruhiwa. © UNSOM

Mji mkuu wa Somalia umeshambuliwa tena na magaidi siku kadhaa baada ya shambulio jingine kugharimu maisha ya watu nchini humo. Mshambuliaji mmoja amejilipua katika jengo la kunakopatikana ofisi ya meya wa mji wa Mogadishu.

Matangazo ya kibiashara

Watu sita wameuawa na wengine sita kujeruhiwa, ikiwa ni pamoja na meya wa Mogadishu.

Wapiganaji wa Al Shabab wameonyesha tena uwezo wao kwa kuingilia katika maeneo ambako ulinzi mkali umeimarishwa. Kulingana na vyanzo kadhaa, mshambuliaji wa kujitoa mhanga aliweza kuingia ndani ya makao makuu ya manispa ya jiji la Mogadishu na kulipua mkanda wake uliojaa vilipuzi katika ofisi ambako meya alikuwa.

Abdirahman Osman alikuwa katika mkutano wa usalama na maafisa kadhaa wa eneo hilo. Bw Osma Amepata majeraha makubwa, na amesafirishwa hospitalini ambapo anasubiri afanyiwe upasuaji. Makamishna wa wilaya ya Abdulaziz na Waberi, ambao wamekuwa wamehudhuria mkutano huo, wameuawa.

Mwakilishi mpya wa Marekani nchini Somalia amekuwa amelengwa na shambulio hilo.

Kundi la Al Shabab limedai kuhusika na shambulio hil na kusema kuwa Mwakilishi mpya wa Marekani James Swan amekuwa amelengwa na shambulio hilo. Mwakilishi mpya wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia, aliyeteuliwa Mei 30, ameponea. Mwanadiplomasia huyo kutoka Marekani alikuwa kwenye jumba la mkutano na meya saa chache kabla ya shambulio hilo.

Katika taarifa iliyorushwa kwenye Twitter, James Swan amelaani shambulio hilo: "Ninasikitishwa na shambulio hio la kutisha ambalo sio tu linahatarisha usalama kwa maisha ya mwanadamu, lakini pia huwalenga Wasomali ambao wanafanya kazi ili kuboresha hali ya maisha ya ndugu zao Wasomali katika mkoa wa Mogadishu-Banadir ".