DRC-USALAMA-HAKI

Visa vya ukiukwaji wa haki za binadamu vyapungua DRC

Ofisi ya timu ya pamoja ya Umoja wa Mataifa inayohusika na masuala ya haki za binadamu imesema vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu vimepungua nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo licha ya kurekodi matukio elfu 3 kati ya mwezi January hadi Juni mwaka huu.

Plisi karibu na kanisa kuu la Notre-Dame Kinshasa, Februari 25, 2018.
Plisi karibu na kanisa kuu la Notre-Dame Kinshasa, Februari 25, 2018. REUTERS/Goran Tomasevic
Matangazo ya kibiashara

Timu hiyo inasema vitendo vya ukiukaji wa haki za binadamu nchini humo vilikuwa vya hali ya juu katika kipindi cha miezi sita tangu rais Felix Tshisekedi aingie madarakani, lakini hata hivyo vimepungua kwa asilimia 8 ukilinganisha na mwaka 2018 katika muda uleule.

Mkurugenzi wa ofisi hiyo ya umoja wa Mataifa, Abdoul Aziz Thioye, amesema angalau sasa kuna ahueni kwa wananchi kutumia haki zao za kikatiba pamoja na haki za kisiasa.

Taarifa hii inakuja wakati ambapo bado wanasiasa kadhaa wa nchi hiyo wamewekwa kwenye orodha ya vikwazo vya umoja wa mataifa kwa tuhuma za kuhusika na vitendo vya ukiukaji haki za binadamu.