LIBYA-WAHAMIAJI-USALAMA

Wahamiaji zaidi ya 100 wafariki dunia katika pwani ya bahari Mediterranean Libya

Wahamiaji wakiokolewa katika Bahari ya Mediterranean na shirka la kihisani la SOS Méditerranée, Juni 12, 2018.
Wahamiaji wakiokolewa katika Bahari ya Mediterranean na shirka la kihisani la SOS Méditerranée, Juni 12, 2018. Karpov / SOS Mediterranee/

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na wahamiaji IOM linasema kuwa zaidi ya wahamiaji 100 wanahofiwa kufa maji baada ya boti waliyokuwa wakisafiria kuzama katika pwani ya bahari Mediterranean nchini Libya.

Matangazo ya kibiashara

Wahamiaji hao wanahofiwa kupoteza maisha baada ya boti yao kuzama wakati wakivuka Pwani ya Libya, tukio linalotajwa kuwa kubwa zaidi kutokea katika Bahari ya Mediteranian kwa mwaka huu

Msemaji wa IOM nchini Libya, Safa Msehli, amesema boti hiyo imezama katika jiji la Khoms, umbali wa kilomita 100 kutoka katika jiji la Tripoli.

Idadi kamili ya miili ya watu waliopoteza maisha bado haijajulikana, huku Msehli akithibitisha kuokolewa kwa wahamiaji 145.

Watu walionusurika kwenye ajali hiyo wanasema boti yao ilikuwa na watu zaidi ya 400.