DRC-USALAMA-HAKI

Watu 700 wauawa ndani ya kipindi cha miezi sita DRC

Wakati wa maandamano dhidi ya utawala wa Joseph Kabila, polisi yawakamata waandamanaji, Januari 19, 2015 Kinshasa.
Wakati wa maandamano dhidi ya utawala wa Joseph Kabila, polisi yawakamata waandamanaji, Januari 19, 2015 Kinshasa. AFP/Papy Mulongo

Mashirika ya kutetea haki za binadamu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo pamoja na yale ya kimataifa, yametoa wito kwa Serikali kuhakikisha watu waliohusika na utekelezaji wa vitendo vya ukiukaji wa haki za binadamu wanapatikana na kushtakiwa.

Matangazo ya kibiashara

Matamshi ya mashirika haya yamekuja wakati huu ripoti iliyotolewa na ofisi ya Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu ikionesha kuwa watu zaidi ya 700 nchini DRC ni waathirika wa vitendo hivyo vilivyotekelezwa kati ya mwezi January na Juni mwaka huu.

Umoja wa Mataifa unasema vyombo vya usalama nchini humo vilihusika na mauaji ya watu karibu 245 huku makundi ya waasi yakihusika na mauaji ya watu zaidi ya 418.

Hayo yanajri wakati katikati ya juma hili ofisi ya timu ya pamoja ya Umoja wa Mataifa inayohusika na masuala ya haki za binadamu ilisema vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu vimepungua nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo licha ya kurekodi matukio elfu 3 kati ya mwezi Januari hadi Juni mwaka huu.

Timu hiyo inasema vitendo vya ukiukaji wa haki za binadamu nchini humo vilikuwa vya hali ya juu katika kipindi cha miezi sita tangu rais Felix Tshisekedi aingie madarakani, lakini hata hivyo vimepungua kwa asilimia 8 ukilinganisha na mwaka 2018 katika muda ule ule.

Wanasiasa kadhaa na baadh ya maafisa wa ngazi ya juu katika vikosi vya usalama na ulinzi nchini Jamhuri ya kidemokrasia ay Congo wamewekwa kwenye orodha ya vikwazo vya Umoja wa Mataifa kwa tuhuma za kuhusika na vitendo vya ukiukaji haki za binadamu.