DRC-SIASA-USALAMA-UCHUMI

Serikali kutangazwa kwa muda wowote DRC

Mambo yameanza kujipa kwa kuundwa serikali ya kwanza ya baada ya Kabila, timu ambayo Sylvestre Ilunga Ilunkamba anatarajia kuongoza kama waziri mkuu. Serikali hiyo inatarajiwa kuundwa na mawaziri 65 kwa jumla.

Rais Felix Tshisekedi (kulia) na Waziri Mkuu mpya Sylvestre Ilunga Ilunkamba.
Rais Felix Tshisekedi (kulia) na Waziri Mkuu mpya Sylvestre Ilunga Ilunkamba. © Présidence de la République démocratique du Congo
Matangazo ya kibiashara

Kwa muda wowote kuanza sasa serikali nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) itatangazwa.

Wajumbe wakuu katika mazungumzo hayo upande wa muungano huo FCC-CACH wamezungumzia pointi mbalimbali zilizogubika mazungumzo hayo mapema usiku, kabla ya kumkabidhi Waziri Mkuu Sylvestre Ilunga Ilunkamba.

Mazungumzo hayo yaliongozwa na Jean-Marc Kabund kwa upande wa muungano wa CACH na Nehemia Mwilanya kwa upande wa FCC chini ya uenyekiti wa Waziri Mkuu Sylvester Ilunga Ilunkamba.

Sherehe hiyo ya urafiki ilidumu dakika chache tu, na kulingana na makubaliano yaliyosainiwa, mawaziri wote sitini na watano watateuliwa kutoka pande zote mbili: muungano wa FCC wa Joseph Kabila na muungano wa CACH wa Félix- Antoine Tshisekedi Tshilombo na Vital Kamerhe. Pande zote mbili zilikubaliana kutawala pamoja katika muungano wao.

Programu ya pamoja ya serikali

Nafasi arobaini na mbili zitapewa mungano wa vyama vinavyo muunga mkono aliyekuwa rais wa DRC Joseph Kabila Kabange, muungano ambao una viti vingi bungeni. Nafasi ishirini na tatu zinazobaki zitapewa muungano wa CACH wa Felix Tshisekedi Tshilombo, muunga ambao uliibuka mshindi katika uchaguzi wa urais wa Desemba 30, 2018.

Ikiwa mpango wa pamoja wa serikali ulitangazwa na kamati ya ufuatiliaji wa utekelezaji wa makubaliano hayo imesainiwa, hakuna taarifa yoyote iliyotolewa kuhusu wizara ambazo kila upande utachukuwa.

Hata hivyo pande zote mbili zinasema kuwa kwa muungano wao huo "wanadhamiria kumaliza umaskini, usiokubalika kwa nchi kama DRC".