DRC-EBOLA-AFYA

DRC: Mgonjwa wa pili wa Ebola afariki dunia Goma

Ebola: Katika kituo cha afya Goma, mashariki mwa DRC, wafanyakazi wakifua mavazi ya kazi na kuosha vifaa vya kazi Julai 17, 2019.
Ebola: Katika kituo cha afya Goma, mashariki mwa DRC, wafanyakazi wakifua mavazi ya kazi na kuosha vifaa vya kazi Julai 17, 2019. REUTERS/Djaffer Sabiti

Mamlaka katika mji wa Goma, Mashariki mwa DRC imethibitisha leo Jumatano kifo cha mgonjwa wa pili aliyepatiana na virusi vya Ebola. Viongozi katika mji huo wamehakikisha kwamba mambo yote yamewekwa sawa ili kutoa chanjo kwa watu wote ambao walisogeleana na mgonjwa huyo.

Matangazo ya kibiashara

Kesi ya kwanza ya Ebola iligunduliwa katikati ya mwezi Julai katika mji wa Goma, mji mkuu wa mkoa wa Kivu Kaskazini, wenye wakaazi milioni mbili. Shirika la Afya Dunia (WHO) wakati huo lilitangaza dharura ya kimataifa ya afya kwa binadamu.

Mwanamume huyo ambaye ni kutoka kijiji cha Mongbwalu katika mkoa wa Ituri, zaidi ya kilomita 600 kaskazini mwa Goma, aliwasili katika mji wa Goma mnamo Julai 13 katika safari ya kuitembelea familia.

Kwa mujibu wa Giscard Kusema, mkurugenzi msaidizi wa vyombo vya habari vya rais, mgonjwa alibaki chini ya uchunguzi wa matibabu ambao uliendelea hadi Jumanne, Julai 30, wakati viongozi walithibitisha kwamba aliambukizwa virusi vya Ebola.

Chanzo hiki kilio karibu na rais kimebaini kwamba kampeni ya kutoa chanjo ilianza Jumatano hii asubuhi katika mji wa Goma kwa watu wote ambao waliweza kuwa na maswasiliano ya karibu na mtu huyu, ili kuzuia maambukizi ya virusi vya ugonjwa huo.