ALGERIA-SIASA-UCHAGUZI

Jeshi lakataa masharti yaliyowekwa na "jopo la wapatanishi" Algeria

Mkuu wa jeshi la Algeria Ahmed Gaïd Salah wakati wa hotuba yake kwenye runinga ya taifa Jumanne, Julai 30, 2019.
Mkuu wa jeshi la Algeria Ahmed Gaïd Salah wakati wa hotuba yake kwenye runinga ya taifa Jumanne, Julai 30, 2019. © Capture d'écran El Bilad TV

Mkuu wa jeshi la Algeria amekataa hatua za kuafikiana zilizoombwa na jopo la wapatanishi ili kuanzisha mazungumzo kuhusu mfumo wa uchaguzi wa urais nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Mazungumzo yanalenga kufanya uchaguzi wa urais "mapema iwezekanavyo," Ahmed Gaïd Salah alisema Jumanne wiki hii. Pamoja na kuwa msimamo huu sio mpya, mkuu wa jeshi la Algeria ameshtumu jithada za mazungumzo.

Alisema maombi ya hatua za kuafikiana ni "Ukoloni mamboleo" na "fikra potovu" ambazo hutoka kwa kile alichokiita "kundi", neno alilotumia kwa kumaanisha wafanyabiashara wakuu walio na ukaribu na familia ya Abdelaziz Bouteflika.

Hatua hizi za kuafikiana, ambazo ni pamoja na kuachiliwa kwa watu waliowekwa kizuizini kwa kuvaa bendera iliyopigwa marufu au kupunguza idadi ya vikosi vya usalama na kutotumia nguvu zaidi wakati wa maandamano, ni maombi kutoka kwa vyama vya kiraia, vyama vya siasa, lakini pia waandamanaji, amesema Ahmed Gaid Salah.

Mchumi Smail Lalmas kujiondoka kwenye "jopo la wapatanishi"

Wakati "jopo la wapatanishi" likiendelea kukosolewa vikali, hoja kuu ya wajumbe wake saba ni kwamba hatua hizi za kuafikiana zilikuwa zimepokelewa vizuri na kaimu rais Abdelkader Bensalah.

Katika muktadha huu, taarifa ya Mkuu wa jeshi inadhoofisha "jopo la wapatanishi" dhidi ya wapinzani na waandamanaji. Jumanne jioni, mmoja wa wajumbe hao, mchumi Smail Lalmas alitangaza kwamba anafikiria kujiondoka kwenye jopo hilo la wapatanishi.