MSUMBIJI-FRELIMO-RENAMO-SIASA

Msumbiji: Serikali na kundi la zamani la waasi RENAMO wasaini mkataba mpya wa amani

Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi (kushoto) na kiongozi wa chama cha RENAMO Ossufo Momade wakisaini mkataba wa amani katika Hifadhi ya Kitaifa ya Gorongoza Agosti 1, 2019.
Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi (kushoto) na kiongozi wa chama cha RENAMO Ossufo Momade wakisaini mkataba wa amani katika Hifadhi ya Kitaifa ya Gorongoza Agosti 1, 2019. Stringer / Office of the President of Mozambique / AFP

Serikali ya Msumbiji, chama tawala nchini humo FRELIMO na kundi la zamani la waasi la RENAMO wametia saini kwenye mkataba mpya wa amani. Kundi la zamani la waasi la RENAMO, sasa ni chama kikuu cha upinzani tangu kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe mnamo mwaka 1992.

Matangazo ya kibiashara

Mkataba huo wa amani ni wa tatu ya amani tangu mwaka 2013, wakati RENAMO ilichukua tena silaha na kuanzisha vita dhidi ya serikali, na umetiliwa saini miezi miwili kabla ya uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika Oktoba 15.

Rais Philipe Nyusi alifanya safari kwenda kwenye ngome ya RENAMO katikati mwa nchi kwa kutia saini kwenye mkataba huo. Serikali iikuwa na nia njema, baada ya kupigiwa kura bungeni Jumatatu wiki hii sheria mpya ya inayotoa msamaha kwa makosa yote yaliyofanywa wakati wa machafuko.

Kwa upande wa Caifadine Manasse, msemaji wa chama tawala FRELIMO, makubaliano haya ni mafanikio halisi ya ahadi ya Rais, kabla ya kutamatisha muhula wake: "Rais alipotawazwa, alijikubalisha kufanya kilio chini ya uwezo wake ili amani inarejea nchini. Lakini kusainiwa kwa mkataba huo, miezi michache kabla ya kumalizika kwa muhula wake, ni thibitisho la kazi nzuri ya rais wa jamhuri. Kazi ya inayowezesha kufikiria chama cha RENAMO ili kuhakikisha kwamba tunaweza sote kuchangia maendeleo ya nchi, " amesema Caifadine Manasse.

Kwa upande wake, Chama cha RENAMO kimeanza mchakato wa kupokonya silaha wapiganaji wake. Kundi hilu la zamani la waasi limekaribisha mkataba huo wa amani ambao, utawezesha uchaguzi ujao unafanyika kwa amani.

Serikali na kundi la waasi la RENAMO walitia saini mkataba wa amani mnamo 1992 ambao ulimaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka 16. Mkataba huu ulikiukwa kati ya mwaka 2013 na 2014. Mkataba wa pili wa amani ulifikiwa mnamo 2014, lakini nao pia ulivunjwa. Mnamo mwaka 2016, kulitangazwa kusitishwa mapigano kufuatia mazungumzo, lakini hakukuwa na mkataba uliosainiwa.