AFRIKA KUSINI-UCHAGUZI-RUSHWA-SIASA

Barua pepe zilizovuja zamuweka mashakani Ramaphosa

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa anaendelea kupinga ripoti ya ofisi ya msimamizi wa mali za umma ambayo ilimtaja kudanganya bunge kuhusu kupokea fedha za michango kusaidia kampeni yake mwaka 2017.
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa anaendelea kupinga ripoti ya ofisi ya msimamizi wa mali za umma ambayo ilimtaja kudanganya bunge kuhusu kupokea fedha za michango kusaidia kampeni yake mwaka 2017. REUTERS/Rodger Bosch

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amesisitiza kuwa hana kosa lolote baada ya kuvuja kwa barua pepe kuhusu mchango aliopokea wakati wa kampeni ndani ya chama cha ANC mwaka 2017.

Matangazo ya kibiashara

Mwishoni mwa mwezi Julai rais Cyril Ramaphosa alisema ataenda mahakamani kupinga ripoti ya ofisi ya msimamizi wa mali za umma ambayo ilimtaja kudanganya bunge kuhusu kupokea fedha za michango kusaidia kampeni yake mwaka 2017.

Kwenye ripoti hiyo Ramaphosa anadaiwa kupokea kiasi cha randi laki 5 kusaidia kampeni zake kinyume na maadili ya utumishi wa uma.

Tayari mkurugenzi wa ofisi ya usimamizi wa mali za uma, Busisiwe Mkhwebane ametoa taarifa akiunga mkono hatua iliyochukuliwa na rais Cyril Ramaphosa.

Awali Ramaphosa aliesema baada ya kuisoma kwa kina alibaini kuwa ripoti hiyo ina makosa na tuhuma za kupikwa na kutaka mara moja ifanyiwe mapitio na mahakama za nchi hiyo.