Pata taarifa kuu
DRC-SIASA

Serikali mpya ya DRC kutangazwa kati ya Agosti 19 na Septemba 7

Rais wa DRCongo Felix Tshisekedi na mtangulizi wake Joseph Kabila katika sherehe ya kuapishwa kwa rais mpya,  Kinshasa Januari 24, 2019.
Rais wa DRCongo Felix Tshisekedi na mtangulizi wake Joseph Kabila katika sherehe ya kuapishwa kwa rais mpya, Kinshasa Januari 24, 2019. REUTERS/ Olivia Acland
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 1

Wananchi wa DRC watalazimika kuwa watulivu na kusubiri kidogo kabla ya kutangazwa baraza jipya la mawaziri katika utawala wa Felix Antoine Tshisekedi Tshilombo, chanzo kilio karibu na ofisi ya rais kimesema.

Matangazo ya kibiashara

Serikali mpya ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo iliyokuwa ikisubiriwa kwa muda mrefu inatarajiwa kutangazwa kati ya Agosti 19 na Septemba 7 mwaka huu, amesema Jeannine Mabunda, Spika wa Bunge la taifa.

Kwa ombi la Rais, Felix Tshisekedi, wabunge wameitishwa kushiriki katika kikao cha cha Jumatatu, Agosti 19 na watajadili kuhusu kuapisha mawaziri hao wapya.

Agosti 14, rais wa DRC alikataa kupitisha timu ya kwanza mawaziri, kwa sababu idadi ya wanawake na vijana haikuwa inatosha.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.