SUDANI-SIASA-USALAMA

Sudan yampata kiongozi mpya

Pande husika katika mgogoro wa Sudan watia saini mkataba wa kuundwa taasisi za mpito, Jumamosi, Agosti 17, 2019.
Pande husika katika mgogoro wa Sudan watia saini mkataba wa kuundwa taasisi za mpito, Jumamosi, Agosti 17, 2019. EBRAHIM HAMID / AFP

Viongozi wa kijeshi na wale wa muungano wa upinzani wametangaza kuundwa kwa baraza huru la uongozi ambalo litatawala kwa mpito katika kipindi cha miaka 3 kuelekea kupata serikali ya kiraia.

Matangazo ya kibiashara

Baraza hilo lenye wajumbe 11, limetangazwa na msemaji wa baraza la mpito la kijeshi ambalo limekuwa likitawala tangu kuangushwa kwa utawala wa Omar al-Bashir mwezi April mwaka huu.

Wakati huu, mchakato wa kuundwa serikali umeanza nchini humo. Orodha ya wajumbe wa kumi na moja watakaoshiriki katika Baraza Kuu Tawala imetangazwa kwenye televisheni na Chamseddine Kabbachi, msemaji wa Baraza la Jeshi la Mpito, jana Jumanne jioni.

Baraza Kuu Tawala litaongozwa kwa kipindi cha miezi 21 na Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, mkuu wa sasa wa Baraza la Jeshi la Mpito ambaye alichukua hatamu ya uongozi wa nchi baada ya rais Omar al-Bashir kutimuliwa madarakani mnamo mwezi Aprili baada ya miongo mitatu madarakani. Rais wa Baraza Kuu Tawala atatawazwa kesho (Jumatano) asubuhi saa 11 mchana," Jenerali Chamseddine Kabbachi alisema.

Kama ilivyoainishwa na makubaliano yaliyotiwa saini Jumamosi kati ya wanajeshi na viongozi wa maandamano, Jenerali al-Burhan atakabidhi madaraka kwa raia kwa kipindi cha mpito cha miezi 18 iliyosalia. Kipindi cha mpito ambacho kitafuata na uchaguzi wa kidemokrasia mnamo mwaka 2022.

Baraza hilo Kuu TAwala litaundwa na raia sita na askari watano.