Pata taarifa kuu
UFARANSA-UJERUMANI-G 5 SAHEL-USALAMA

Ufaransa na Ujerumani zaungana na nchi zingine kwa kuimarisha kikosi cha G5 Sahel

Kufuatia mkutano wa G7 uliozungumzia kuhusu hali barani Afrika, Rais wa Burkina Faso Kaboré, Rais wa Ufaransa Macron na Kansela wa Ujerumani Merkel wamefanya mkutano na waandishi wa habari.
Kufuatia mkutano wa G7 uliozungumzia kuhusu hali barani Afrika, Rais wa Burkina Faso Kaboré, Rais wa Ufaransa Macron na Kansela wa Ujerumani Merkel wamefanya mkutano na waandishi wa habari. © Ian LANGSDON / POOL / AFP
Ujumbe kutoka: RFI
2 Dakika

Kwa kukabiliana na kile Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ameita "kuongezeka na kupanuka kwa tishio la kigaidi katika ukanda wa Sahel", Paris na Berlin wametangaza kuunga mkono zaidi kikosi cha kimataifa cha G5 Sahel. Lakini pia wametoa wito kwa ushirikiano mpya ulio "mpana" kwa nchi jirani za Ukanda huo.

Matangazo ya kibiashara

Wakizungumza kwenye mkutano wa kilele wa G7, Emmanuel Macron na Angela Merkel wameelezea juu ya umuhimu wa kutoa msaada wa silaha na kutoa mafunzo bora ya kijeshi kwa jeshi na polisi vya Ukanda wa Sahel. Lakini pia wamebaini kwamba ni muhimu kusaidia nchi za Ukanda wote huo. Wanatambua kuwa nchi nyingi za ECOWAS (Jumuiya ya Uchumi wa nchi za Magharibi) zinaathiriwa kwa njia moja ama nyingine na ukosefu wa usalama katika Ukanda wa Sahel.

Rais Macron amebaini kwamba kuna haja ya kufafanua tena "eneo la usalama". Ufaransa na Ujerumani zinataka kuhusisha nchi za Ghuba ya Guinea, haswa Senegal, Cote d'Ivoire na Ghana, kwa juhudi za kikosi cha G5 Sahel.

Nguvu ya hatua iliyochukuliwa leo ni kuongeza eneo la usalama ikilinganishwa na kuongezeka au kupanuka kwa ugaidi, na haswa, itawezesha kuwashirikisha tena katika nyanja ya usalama wanachama wa ECOWAS.

Uungwaji huu mkono wa nchi za pwani ya Afrika Magharibi ni hatua ya kupongezwa. Lakini kwa malengo gani hasa? Hii haijawekwa wazi kabisa. Kimsingi, jambo hili litaamuliwa wakati wa mkutano kati ya Ufaransa na Ujerumani kabla ya mwisho wa mwaka huu.

Mkutano wa kilele wa ECOWAS ambao utafanyika katikati mwa mwezi Septemba katika mji mkuu wa Burkina Faso, Ouagadougou, utajadili kuhusu kuundwa kwa muungano mpana wa kjeshi utakaojumuisha nchi zenye askari katika kikosi cha G5 Sahel na baadhi ya majirani zao.

Rais wa Cote d'Ivoire Alassane Ouatarra, tayari ametoa wito wa "kuungana" kati ya G5 Sahel, Cédéao na Afrika ya Kati, akibaini kwamba Cameroon iko tayari kushiriki.

Kwa upande wake, Rais Kaboré wa Burkina Faso, aliyealikwa katika mkutano wa G7, amekumbusha umuhimu wa kupata suluhisho la kisiasa kwa mzozo wa Libya, suala ambalo linaendana na ukosefu wa usalama katika Ukanda wa Sahel.

Ni genge ambalo linapanuka na tumeona ni muhimu washirika wote wapate suluhisho la swali la Libya ambalo litatuwezesha kumaliza kusambaa kwa ugaidi sio tu katika Ukanda wa Saheli lakini pia katika nchi za pwani, " amesema Roch Marc Christian Kaboré

Kwa upande wa Angela Merkel, hata hivyo, amesema hakuna haja ya kutuma askari zaidi katika Ukanda wa Sahel. Karibu askari 200 wa Ujerumani tayari wanashirijki katika ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Mali. Kwa mtazamo wa Berlin, "hiyo inatosha".

Kwa sasa, Ufaransa na Ujerumani bado zinajaribu kuwashawishi wafadhili wengine na sio tu kwa wanachama wa G7 kujitolea katika ushirikiano huu mpya kwa Ukanda wa Sahel.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.