Pata taarifa kuu
GUINEA BISSAU-SIASA-USALAMA

Guinea-Bissau: Rais Vaz kuwania muhula wa pili

Rais Vaz alichaguliwa mnamo mwaka 2014, alimaliza muhula wake wa miaka mitano kama rais wa Guinea-Bissau Juni 23.
Rais Vaz alichaguliwa mnamo mwaka 2014, alimaliza muhula wake wa miaka mitano kama rais wa Guinea-Bissau Juni 23. © SEYLLOU / AFP
Ujumbe kutoka: RFI
2 Dakika

Rais wa Guinea-Bissau anaye maliza muda wake, José Mario Vaz, ametangaza kwamba atawania muhula wa pili katika uchaguzi wa urais nchini humo ambao umepangwa kufanyika Novemba 24.

Matangazo ya kibiashara

Rais Vaz amesema kuwa atawania kama mgombea binafsi. "Nitawania katika uchaguzi ujao wa urais. Nitakuwa mgombea anayetetea amani na utulivu, "Rais José Mario Vaz amewaambia maelfu ya wafuasi wake kutoka nchi nzima Alhamisi jioni wiki hii.

Rais José Mario Vaz anaungwa mkono na vyama vidogo vidogo ambavyo haviwakilishwi bungeni.

Rais José Mario Vaz ambaye ametengwa na chama chake cha PAIGC kiliyomuweka madarakani mnamo mwaka 2015, katika uchaguzi huu, atawania kama mgombea binafsi.

José Mario Vaz, 62, ndiye rais pekee akitawala kwa kipindi cha miaka 25 anakamilisha muhula wake. Watangulizi wake waliangushwa madarakani kupitia mapinduzi ya kijeshi na wengine waliuawa. Kuuwa huchukuliwa kama njia nyingine ya kufanya siasa katika nchi hii ndogo inayoongea Kireno.

Guinea-Bissau, ni nchi ambayo inaendelea kukabiliwa na mgogoro wa kisiasa kwa miaka kadhaa.

José Mario Vaz atachuana na wagombea wengine watano: Domingos Simoes Pereira, Waziri Mkuu wa zamani na kiongozi wa Chama cha PAIGC, ambacho kinaongoza katika siasa ya Guinea-Bissau tangu nchi hiyo ijipatie uhuru mnamo mwaka 1974. Wawili hao wanapingana tangu kuibuka kwa mzozo wa mwaka 2015 wakati rais José Mario Vaz alimwachisha kazi waziri wake mkuu, Domingos Simoes Pereira.

Wagombea wengine wanaowania kinyang'aniro hicho cha urais ni Waziri Mkuu wa zamani Carlos Gomes Junior, kama mgombea binafsi, Umaro El Mokhtar Sissoco Embalo, atapeperusha pendera ya chama cha Madem na Nuno Gomes Nabiam, mgombea wa urais aliyeshindwa katika uchaguzi wa urais wa mwaka 2015.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.