Pata taarifa kuu
DRC-UN-USALAMA-SIASA

Guterres: Upepo mpya wa matumaini na hali bora unavuma DRC

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, akutana Jumatatu, Septemba 2, 2019 na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Félix-Antoine Tshisekedi.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, akutana Jumatatu, Septemba 2, 2019 na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Félix-Antoine Tshisekedi. MONUSCO/John Bompengo

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametamatisha ziara yake ya siku tatu nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo baada ya kuzuru maeneo kadhaa ikiwemo Goma na kukutana na viongozi mbalimbali wa serikali lakini pia wanasiasa.

Matangazo ya kibiashara

Katika hata ya mwisho ya ziara yake nchini DRC, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, alikutana na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Félix-Antoine Tshisekedi. Wawili hawa walijadili masuala mengi, ikiwa ni pamoja na vita dhidi ya ugonjwa wenye virusi vya Ebola, ukosefu wa usalama mashariki mwa DRC, hali ya kibinadamu nchini humo, na marekebisho ya muhula wa Monusco.

António Guterres ametowa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuunga mkono juhudi za Kongo katika kukuza demokrasia.

Wakati akikutana na spika wa bunge Jeanine Mabunda na wenyeviti wa makundi ya wabunge, Guterres amebaini kuwa kipaombele cha serikali ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo ingelipashwa kuwa udhibiti kuhusu unyonyaji wa maliasili. Pia aliomba uimarishaji wa ushirikiano kati ya DRC na MONUSCO,

Guterres amesema kama angeliweza kuchaguwa kipaombele kwa hatua ya serikali na msaada wa jumuiya ya kimataifa, ingelikuwa ni udhibiti wa serikali kwa kila kinachoendelea kuhusu unyonyaji wa rasilimali

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa ametetea hoja yake hiyo kwamba hatua hiyo sio tu kwamba itaongeza mapato kwa serikali, lakini pia itakomesha ufadhili kwa makundi ya waasi yanayotekeleza mauji ya kutisha.

Antonio Guterres amesema amekutana na washikadau mbalimbali nchini humo wakiwemo viongozi wa serikali, wabunge wa upinzani na wale wa utawala na kuwa na matumaini kwamba watetekeleza jukumu kuhakikisha matumaini yalipo yanawanufaisha wananchi wa Congo.

Amesema kwamba anahitaji kuona serikali inaongeza ushirikiano.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.