Pata taarifa kuu
CONGO-UFARANSA-USHIRIKIANO

Rais wa Congo Denis Sassou Nguesso azuru Ufaransa

Rais wa Congo, Denis Sassou-Nguesso.
Rais wa Congo, Denis Sassou-Nguesso. EVGENIA NOVOZHENINA / POOL / AFP
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 2

Rais wa Congo Brazaville Denis Sassou Nguesso anafanya ziara ya kikazi nchini Ufaransa, na anatarajia kukutana kwa mazungumzo na mwenyeji wake, rais Emmanuel Macron, katika Ikulu ya Elysee. Mara ya mwisho viongozi hao kukutana ilikuwa ni Novemba mwaka 2018.

Matangazo ya kibiashara

Duru za ikulu ya rais zinaeleza kuwa mazungumzo kati ya marais hao, Emmanuel Macron na Denis Sassou Nguesso yanatarajia kugubikwa na maswala ya mabadiliko ya hali ya hewa, uchumi, siasa za ndani nchini Congo pamoja na hali nchini Libya.

Wakati huu msitu wa Amazonia ukiendelea kuteketea, Congo ambayo inachukuwa asilimia 10 ya msitu wa bonde la Congo, lazima uvutie zaidi umakini kutoka jumuiya ya kimataifa kwa ajili ya kulinda chanzo cha pili cha ikologia duniani.

Ziara hiyo ya Rais Sassou Nguesso jijini Paris inakuja ikiwa ni miezi miwili baada ya kusainiwa kwa makubaliano kati ya nchi yake na fuko la fedha duniani IMF. Ufaransa ilikuwa imeweka masharti ya msaada wa zaidi ya Faranga za cefa bilioni 88, jambo ambalo kwa serikali ya Brazaville imekuwa ni kikwazo kutokana na kwamba inatakiwa kutekeleza hatua 48 ya masharti iliopewa.

Duru za kidiplomasia zimeeleza kuwa sasa njia iko wazi kwa ajili ya kutolewa kwa msaada huo kutoka Paris, zikisema kwamba kunatarajiwa kusainiwa makubaliano ya ushirikiano wakati wa ziara hiyo ya Rais Sassou Nguesso nchini Ufaransa.

Viongozi hao wawili huenda wakazungumzia pia siasa, uchaguzi wa urais wa mwaka 2021 nchini Congo ambapo Katiba iliyopitishwa kwa tabu mwaka 2015 inamruhusu Sassou Nguesso kuwania upya uchaguzi ujao wa mwaka 2021.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.