AFRIKA KUSINI-USALAMA

Afrika Kusini yaahidi kutokomeza mashambulizi dhidi ya wageni

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa kwenye makao makuu ya Bunge, Cape Town, 20, 2019 (picha ya kumbukumbu).
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa kwenye makao makuu ya Bunge, Cape Town, 20, 2019 (picha ya kumbukumbu). REUTERS/Rodger Bosch

Watu watano wameuawa nchini Afrika Kusini kutokana na mashambulizi yanayoendelea kuwalenga wageni wanaoishi nchini humo, hasa kutoka Nigeria na Zambia.

Matangazo ya kibiashara

Maduka ya raia wa kigeni yamevamiwa na bidhaa zao kuchukuliwa, na sasa yamesalia matupu.

Hata hivyo, duka la Sabastiane raia wa Afrika Kusini halikuguswa.

“Waliamua kulenga maduka ya wageni kutoka DRC na Pakistan. Hawakugusa maduka ya raia wa Afrika Kusini. Wamefanya vibaya sana kwa sababu wageni hawa wana bidii, angalia maduka yao, hayana kitu sasa hivi, “ amesema Sabastiane.

“Afrika Kusini ina wageni wengi sana.Unaweza kufikiri ndipo kituo cha wakimbizi duniani. Nani anastahili kuwalinda, “ Sivuyile Nama, msemaji wa kundi la watu waliovamia maduka ya wageni, ametetea kitendo hciho.

Waziri anayeshughulikia maswala ya Polisi Bheki Cele anasema wanapambana na watu wanaoshambulia maduka ya wageni.

“Kwangu huu ni uhalifu, lakini siwezi kusema kuna kitu kinachonifanya nisema ni raia wa Afrika Kusini kuwavamia wageni.Tunazungumzia uhalfu sio raia wa kigeni kuvamiwa, “ Bheki Cele amesema.

Rais Cyril Ramaphosa amelaani mashambulizi dhidi ya wageni na uvamizi wa maeneo yao ya biashara jijini Johhanersburg.

Kiongozi huyo kupitia ujumbe aliotuma kwenye ukura wake wa Twitter, amesema mashambulizi hayo hayakubaliki.