MSUMBIJI-PAPA FRANCIS-MAJANGA ASILI

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani azuru Msumbiji

Papa Francis akiingia katika ndege kwenye Uwanja wa Ndege wa Fiumicino kwa ziara yake ya kihistoria katika nchi tatu za Afrika, Roma Septemba 4, 2019.
Papa Francis akiingia katika ndege kwenye Uwanja wa Ndege wa Fiumicino kwa ziara yake ya kihistoria katika nchi tatu za Afrika, Roma Septemba 4, 2019. Vatican Media/­Handout via REUTERS

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis ameanza ziara ya kihistoria nchini Msumbuji, na kulakiwa na mamia ya watu katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Maputo na kupokelewa na rais Filipe Nyusi.

Matangazo ya kibiashara

Hii ni ziara ya kwanza ya kiongozi wa Kanisa hilo nchini Msumbiji baada ya kiongozi wa zamani John Paul wa pili kufanya hivyo mwaka 1988.

Baada ya Msumbiji atakwenda Madagascar na Maurituis katika ziara anayokuja kuhimiza amani, lakini pia kuhamasisha vita dhidi ya umasikini.

Kiongozi huyo anatarajiwa kufanya ziara ya wiki moja kutembelea nchi za Afrika ambazo zimekumbwa na umaskini, vita na majanga ya asili zikiwamo Madagascar, Mauritius na Msumbiji ambazo zilitembelewa na papa John Paul II mwaka 1988 na 1999.

Katika siku ya kwanza ya ziara yake nchini Msumbiji, Papa Francis anatarajia kuzungumzia mambo mbalimbali ikiwamo tatizo la umaskini katika nchi za Afrika, uhifadhi wa mazingira na ufisadi.

Papa Francis anatarajia kusfiri kwenda Madagascar kesho Ijumaa. Raia nchi humo wanajiandaa kwa ziara hiyo ya kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani.