NIGERIA-AFRIKA KUSINI-USALAMA

Nigeria yasusia mkutano wa kiuchumi wa dunia Afrika Kusini

Polisi wakipiga doria katika eneo jirani na Alexandra, Johannesburg, ambapo ghasia na uporaji dhidi ya mali za wageni vimekuwa vikiendeshwa. Septemba 3, 2019.
Polisi wakipiga doria katika eneo jirani na Alexandra, Johannesburg, ambapo ghasia na uporaji dhidi ya mali za wageni vimekuwa vikiendeshwa. Septemba 3, 2019. © REUTERS/Marius Bosch

Nigeria imesema haitatuma mwakilishi katika mkutano wa kiuchumi wa dunia unaoendelea nchini Afrika Afrika, kufuatia mashambulizi na uvamizi unaendelea kulenga maduka ya wageni nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Makamu wa rais Yemi Osinbajo alitarajiwa kuhotubia mkutano huo mjini Cape Town leo Alhamisi lakini hatakuwepo.

Watu zaidi ya sita wameauwa kutokana na vurugu hizi zilizoanza kushuhudiwa wiki hii, jijini Johannerburg na baadaye kwenda jijini Pretoria.

Nchini Nigeria, Jumatano wiki hii kulikuwa na maandamano, raia wa jiji kuu Abuja wakiandamana na kuvamia maduka ya wawekezaji kutoka Afrika Kusini kama MTN na duka la jumla la Shoprite, kwa kile walichosema ni kulipiza kisasi.