Pata taarifa kuu
ZIMBABWE-MUGABE-SIASA

Rais wa zamani wa Zimbabwe Robert Mugabe afariki dunia

Rais wa zamani wa Zimbabwe Robert Mugabe katika mkutano na waandishi wa habari wakati huo alitangaza kwamba hatapigia kura chama cha Zanu-PF Julai 29, 2018.
Rais wa zamani wa Zimbabwe Robert Mugabe katika mkutano na waandishi wa habari wakati huo alitangaza kwamba hatapigia kura chama cha Zanu-PF Julai 29, 2018. REUTERS/Siphiwe Sibeko
Ujumbe kutoka: RFI
2 Dakika

Rais wa zamani wa Zimbabwe ambaye ni muasisi na Baba wa Taifa hilo, Robert Mugabe amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 95. Alikuwa amelazwa hospitalini nchini Singapore kwa miezi mitano.

Matangazo ya kibiashara

Robert Mugabe ambaye alitawala Zimbabwe tangu uhuru wa nchi hiyo mnamo mwaka 1980, alilazimika kujiuzulu mnamo mwezi Novemba 2017 kwa shinikizo la jeshi na chama chake, ZANU-PF.

Nafasi yake ilichukuliwa na makamu wake wa zamani, Emmerson Mnangagwa, aliyechaguliwa tena kama rais wa Zimbabwe mnamo mwezi Julai 2018.

"Ni kwa huzuni mkubwa ninatangaza kifo cha baba wa taifa na muasisi wa uhuru wa Zimbabwe na rais wa zamani, kamanda Robert Mugabe," Rais wa sasa wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa, ameandika ujumbe kwenye ukurasa wake wa twitter.

“Mugabe alikuwa alama ya ukombozi. Mpigania uhuru wa Afrika aliyejitolea maisha yake kwa ajili ya kuwainua watu. Mchango wake kwa Taifa hili na Bara hili hautasahaulika. Roho yake ipumzike kwa amani,” ameongeza.

Mugabe alikuwa anasumbuliwa na maradhi ambayo hayakuwahi kuwekwa wazi. Alikuwa akipatiwa matibabu nchini Singapore mara kadhaa, lakini alipatiwa matibabu mfululizo nchini humo tangu Aprili mwaka huu.

Hata hivyo Rais Emmerson Mnangagwa amebaini kwamba Mugabe alikuwa anasumbuliwa na maradhi pamoja na uzee..

Mugabe alilazimika kujiuzulu baada ya kupata shinikizo kutoka kwa jeshi na maafisa wakuu wa chama chake cha Zanu-PF, baada ya kuongoza chama hicho kwa miaka 37. Jeshi lilimtaka ajiuzulu baada ya kutokea malumbano kati yake na makamu wake ambaye ni rais wa sasa Emmerson Mnangagwa, aliefutwa kazi na kukimbilia uhamishoni, kabla ya kurejea nchini kuchukua nafasi ya mtangulizi wake.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.