Pata taarifa kuu
SUDANI-SIASA-USALAMA

Sudani: Serikali ya kwanza baada ya Bashir yatangazwa

Waziri Mkuu Abdallah Hamdok atangaza baraza lake la mawaziri katika mkutano na waandishi wa habari, Khartoum Septemba 5, 2019.
Waziri Mkuu Abdallah Hamdok atangaza baraza lake la mawaziri katika mkutano na waandishi wa habari, Khartoum Septemba 5, 2019. © Ebrahim HAMID / AFP
Ujumbe kutoka: RFI
2 Dakika

Waziri Mkuu wa Sudani, Abdallah Hamdok, ametangaza majina ya wajumbe wa baraza lake la mawaziri, hatua ya kipindi cha mpito baada ya Omar al-Bashir kutimuliwa mamlakani mnamo mwezi Aprili.

Matangazo ya kibiashara

"Ni mwanzo wa enzi mpya. Ikiwa tutafanikiwa, Sudani mpya itajengwa, "Waziri mkuu amesema Alhamisi jioni wiki hii katika mkutano na waandishi wa habari.

Baraza hili la mawaziri lina wajumbe 18 na Waziri Mkuu ana haki ya kuteua majina ya watu mawili baadaye, sawa na wajumbe ishirini kwa jumla, kama ilivyoainishwa katika makubaliano yaliyofikiwa kati ya pande jeshi na viongozi wa maandamano. Wanawake wanne, ikiwa ni pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje, Asma Mohamed Abdallah, ni miongoni mwa mawaziri hao. Hii ni kwa mara ya kwanza kwa nchi hii hata kama wiki mbili zilizopita, chama cha wanawake kilidai kuepo na usawa kati ya wanaume na wanawake katika serikali hiyo mpya. "Ni sawa kuwa na wanne tu? Kwa kweli sivyo. Lakini ni mwanzo mzuri, "amesema Abdalla Hamdok.

Waziri Mkuu wa Sudani amemteua Waziri wa Fedha Ibrahim Elbadawi, mchumi wa zamani katika Benki ya Dunia. Walakini, mbabe wa mapinduzi, Maddani Abbas Madani, ameteuiwa kuwa Waziri wa Biashara na Viwanda.

Kama ilivyopangwa, Baraza la kijeshi limewateua , Luteni Jenerali Gamal Omar kama Waziri wa Ulinzi, na Idriss Traifi kama Waziri wa Mambo ya Ndani.

Hatua hii inakuja miezi michache baada ya jeshi na viongozi wa maandamano kufikia mkataba wa kihistoria wa kugawana madaraka.

Serikali ya mpito ya Sudan itafanya kazi chini ya usimamizi wa Baraza la Utawala wa Mpito litakaongozwa na wajumbe 11 wakiwemo sita wa kiraia na wanajeshi watano; na litaongoza kwa muda wa miaka 3 kuelekea uchaguzi mkuu.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.