CAMEROON-SIASA-USALAMA

Rais wa Cameroon Paul Biya aitisha mazungumzo ya kitaifa

Le président camerounais Paul Biya lors de ses voeux à la nation, le 31 décembre 2018.
Le président camerounais Paul Biya lors de ses voeux à la nation, le 31 décembre 2018. © RFI/Capture d'écran

Rais wa Cameroon Paul Biya amewataka wadau wote katika mgogoro unaendelea nchini humo kuketi kwenye meza ya mazungumzo ili kutafutia suluhu mgogoro huo.

Matangazo ya kibiashara

Paul Biya mesemak atika hotuba kwa taifa kwamba mazungumzo hayo yanapaswa kuitishwa haraka kabla ya mwisho wa mwezi huu wakati nchi hii inaendelea kukumbwa mdororo wa usalama kwa karibu miaka miwili kutokana na machafuko yanayoendelea katika eneo lonalozungumza Kiingereza. Machafuko hayo mpaka sasa yamesababisha vifo vya watu 2,000, kwa mujibu wa mashirika ya haki za binadamu.

Tangazo la kuitisha mazungumzo ya kitaifa limecheleweshwa katika hotuba ya rais Biya kwa taifa. tangazo hilo limetolewa katika dakika ya ishirini ya hotuba hiyo ambayo ilidumu dakika thelathini.

"Mazungumzo haya yatatuwezesha kutathmini njia na uwezo wa kujibu madai ya wakaazi wa kaskazini magharibi na kusini magharibi mwa Cameroon," Rais Paul Biya amesema.

Wazo hilo sio jipya, kwani lilipendekezwa kwa muda mrefu na wanasiasa mbalimbali ndani na nje ya nchi hiyo, Paul Biya amesema, huku akipinga dhidi ya uchanganuzi kuhusu chanzo cha mgogoro: "Kushindwa kwa jitihada hizi kulitokana kwa wakati mwingine au kwa bahati mbaya maoni potovu ya wanaharakati wanaotaka maeneo yao kujitenga na kuwa nchi huru, " amebaini Rais Paul Biya.

"Mazungumzo haya yatawaleta pamoja "wadau wote katika maendeleo na usalama wa nchi hii", ikiwa ni pamoja na wawakilishi wa vikosi vya ulinzi na usalama, na vile vile makundi ya watu wenye silaha na waathiriwa.

Waziri Mkuu, Joseph Dion Nguté, MBye kutoka kusini-magharibi mwa nchi ndio atakayeongoza mazungumzo hayo, baada ya kufanya mashauriano, kwa mujibu wa rais Paul Biya.

"Mustakabali wa ndugu zetu wa kaskazini magharibi na kusini magharibi uko katika Jamhuri yetu. Cameroon itabaki moja na haitagawanyika, " ameongeza Paul Biya.

"Ni ishara nzuri, lakini bado masuali mengi yanahitajika katika mazungumzo haya, suala kama lile la shirikisho," amesema Jean Tsomelou, katibu mkuu wa chama cha Social Democratic Front, chama kikuu ambacho wajumbe wake wengi wanatoka katika maeneo kunakozungumzwa Kiingereza nchini Cameroon.

Tangazo hilo linakuja wiki tatu baada ya kiongozi wa wa wanaharakati wanaotaka maeneo yao kujitenga na kuwa nchi huru, Julius Ayuk Tabe na wafuasi wake tisa kuhukumiwa kifungo na wakati viongozi kadhaa wa upinzaji nchini Cameroon wanakabiliwa na kwenye kesi ya kuanzisha uasi.