ZIMBABWE-MUGABE-SIASA

Mugabe kuzikwa baada ya mwezi mmoja

Mwili wa Mugabe umerejeshwa nchini Zimbabwe kwa mazishi yake ya kitaifa.
Mwili wa Mugabe umerejeshwa nchini Zimbabwe kwa mazishi yake ya kitaifa. © AFP

Mwili wa rais wa zamani wa Zimbabwe Ribert Mugabe leo Jumatatu utaplekwa katika kijiji alichozaliwa cha Kutama, kutoa nafasi kwa waakazi wa eneo hilo kutoa heshima zao za mwisho.

Matangazo ya kibiashara

Mwishoni mwa wiki iliyopita, kulikuwa na ibada ya kumkumbuka Mugabe iliyofanyika katika uwanja wa Michezo jijini Harare na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa bara la Afrika.

Rais wa sasa Emmerson Mnagagwa alimtaja Mugabe kama kiongozi aliyekuwa na maono na kusema kwamba 'taifa letu linalia'.

Mazishi ya Mugabe yalitarajiwa kufanyika Jumapili Septemba 15, lakini mpango huo uilionekana kufutiliwa mbali.

Mugabe aliyefariki nchini Singapore akiwa na umri wa miaka 95 wiki mmili zilizopita, atazikwa baada ya mwezi mmoja katika makaburi ya mashujaa jijini Harare.