Pata taarifa kuu
COTE D'IVOIRE-ICC-GBAGBO-HAKI

Mwendesha mashtaka wa ICC akata rufaa dhidi ya kuachiliwa huru kwa Gbagbo na Blé Goudé

Waziri wa zamani wa Vijana Charles Blé Goudé (kushoto) na rais wa zamani wa Cote d'Ivoire, Laurent Gbagbo (kulia).
Waziri wa zamani wa Vijana Charles Blé Goudé (kushoto) na rais wa zamani wa Cote d'Ivoire, Laurent Gbagbo (kulia). © Peter Dejong / POOL / AFP/ Montage RFI

Mwendesha mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) Fatou Bensouda,  amekata rufaa leo Jumatatu, Septemba 16 dhidi ya kuachiliwa huru kwa Laurent Gbagbo na Charles Blé Goudé, mwenyekiti wa zamani wa kundi la Vijana kutoka chama tawala cha zamani nchini Côte d'Ivoire.

Matangazo ya kibiashara

Mwendesha mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu Fatou Bensouda amebaini kwamba majaji wangelisubiri kutoa uamuzi wao na sio kuawaachiliwa huru.

Mwezi Januari mwaka huu, majaji wa ICC waliwaachilia huru wawili hao, wakielezea ushahidi usiotosha na wenye udhaifu ambao uliwasilishwa na upande wa mashitaka, hoja ambayo kwa sasa Fatou Bensouda amepinga.

Tofauti hiyo ni muhimu: Kuaachilia huru wawili hao wakati kutochukua hukumu yoyote inaonyesha jukumu la kila mmoja katika uhalifu wanaoshtumiwa, ikiwa ni pamoja na uhalifu dhidi ya binadamu katika mzozo ambao ulizuka baada ya uchaguzi wa urais wa mwaka 2010, amesema Fatou Bensouda.

Utaratibu wa mahakama sasa utachukuwa muda mrefu kama kawaida kwa mahakama ya ICC.

Rais wa zamani wa Cote d'Ivoire, ambaye bado yuko Brussels chini ya usimamizi wa mahakama, hadi sasa hajaruhusiwa na ICC kuondoka mji mkuu wa Ubelgiji.

Licha ya kuachiliwa huru, Laurent Gbagbo amewekwa chini ya usimamizi wa mahakama na hawezi kuondoka nje ya mji mkuu wa Ubelgiji bila idhini ya mahakama. Vivyo hivyo kwa Charles Blé Goudé ambaye bado yuko mjini Hague.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.