DRC-UBELGIJI-USHIRIKIANO

Rais wa DRC Felix Tshisekedi kuzuru Ubelgiji

Rais wa DRC Felix Tshisekedi atawasili Brussels kwa ziara ya kiserikali Septemba 16 (picha ya kumbukumbu).
Rais wa DRC Felix Tshisekedi atawasili Brussels kwa ziara ya kiserikali Septemba 16 (picha ya kumbukumbu). © AFP

Rais wa DRC Felix Tshisekedi Tshilombo anatarajia kuzuru Ubelgiji Jumatatu hii, ikiwa ni hatua ya kwanza ya ziara ya kiserikali katika nchi hiyo tangu kuchukuwa hatamu ya uongozi wa nchi hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Atasafiri na ndege yake binafsi na atapokelewa kwa heshima kwenye uwanja wa ndege wa Melsbroek, karibu na mji wa Brussels. Ziara hii ina lengo la kuboresha uhusiano kati ya DRC na Ubelgiji. Hii ni ziara ya kwanza ya kiserikali ya Félix Tshisekedi barani Ulaya.

Ubelgiji imekaribisha ziara hii ya rais wa DRC, kwa sababu, kwa upande wake, inamaanisha kwanza kwamba uhusiano kati ya nchi hizo mbili hatimaye umerudi kuwa mzuri na pili uhusiano na nchi hiyo ya kifalme unaelezwa na rais Felix Tshisekedi kuwa ni muhimu sana.

Ubelgiji, hata hivyo, kwa miezi kadhaa haikuonyesha msimamo wowote kuhusina na matokeo ya uchaguzi wa urais, ambapo Rais Fekix Tshisekedi alitangazwa mshindi.. licha ya nchi kadhaa za Ulaya kulalamika kuhusu kasoro zilizojitokewa katika uchaguzi huo.

Lakini mabadiliko haya ya kwanza ya amani katika uongozi wa nchi tangu uhuru wa nchi hiyo yalikuwa yanahitajika kwa kufunua ukurasa mpya kwa uchaguzi, ili kutoa nafasi ya mabadiliko hayo, kwa mujibu wa Ubelgiji.

Rais Tshisekedi anatarajiwa kukutana kwa mazungumzo na mfalme wa Ubelgiji Jumanne wiki pamoja na Waziri Mkuu na mawaziri mbalimbali wa serikali ya Ubelgiji.

Ziara hii ya kiserikali inalenga kufufua ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.

Mikataba minne inatarajiwa kusainiwa kati ya nchi hizo mbili ili kuzindua misaada kwa taasisi mbalimbali za DRC, ili kufufua ushirikiano wa kijeshi, miradi ya ushirikiano wa maendeleo pamoja na uhusiano wa kidiplomasia.