DRC-RWANDA-WAASI-SIASA

Pacific Ntawunguka atajwa kiongozi mpya wa kundi la FDLR

Waasi wa FDLR
Waasi wa FDLR AFP PHOTO/ Tony KARUMBA

Kundi la waasi la FDLR limemtaja Pacific Ntawunguka kuwa kiongozi wake mpya, baada ya kuuawa kwa Sylvestre Mudacumura wiki hii Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Matangazo ya kibiashara

Ntawunguka alikuwa msaidizi wa muda mrefu wa Mudacumura, kabla ya kuuliwa kwake na wanajeshi wa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Wachambuzi wa mzozo wa Mashariki mwa DRC wanamwelezea kiongozi huyu mpya wa FDLR kama rubani wa ndege za kivita mwenye uzoefu na vita, na kumrithi Mudacumura kulitarajiwa.

Kundi la FDLR, limekuwa likisababisha ukosefu wa usalama katika eneo la Mashariki mwa nchi hiyo kwa miaka 25 na kusababisha vifo vya maelfu ya watu.