Pata taarifa kuu
DRC-EBOLA-AFYA-WHO-CHANJO

WHO: Chanjo ya pili ya Ebola nchini DRC kuanza kutolewa mwezi Oktoba

Chanjo ya kwanza ikitolewa mjini Goma mwezi Agosti
Chanjo ya kwanza ikitolewa mjini Goma mwezi Agosti Augustin WAMENYA / AFP
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 2

Shirika la afya duniani WHO limetangaza kuwa chanjo ya pili dhidi ya ugonjwa wa Ebola itatolewa kuanzia katikati ya mwezi wa Oktoba katika eneo la Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Matangazo ya kibiashara

Tangazo limekuja wakati huu Shirika la Madaktari wasiokuwa na mipaka likiishtumu WHO kwa kutoa kiwango kidogo cha chanjo ya kwanza ambayo haikuwafikia watu wengi kama ambavyo ilitarajiwa.

WHO pamoja na Wizara ya afya nchni DRC, zimetangaza mpango huo baada ya kuthibitisha kuwa chanjo hiyo ya pili iliyotengezwa na kampuni ya Johnson & Johnson, ni salama kwa binadamu.

Hii ni chanjo ambayo ilikuwa imepingwa na Waziri wa zamani wa afya Olly Ilunga ambaye alijiuzulu kwa madai kuwa chanjo hiyo haikuwa imefanyiwa majaribio.

Baada ya kujiuzulu, Ilunga alifunguliwa mashtaka ya kufuja fedha zilizokuwa zimetolewa na serikali kupambana na ugonjwa huo hatari.

Matshidiso Moeti, Mkurugenzi wa WHO barani Afrika amesema chanjo hiyo ya pili, itasaidia sana kudhibiti maambukizi hayo ambayo yameendelea kuzua wasiwasi Mashariki mwa DRC na nchi jirani.

Wiki iliyopita, WHO ilisema kuwa idadi ya watu waliopoteza maisha kutokana na Ebola kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita, imefikia 2,103 huku wengine 3,145 wakiambukizwa.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.