Pata taarifa kuu
ZIMBABWE-MUGABE-SIASA

The Herald: Saratani ndio iliyomuua Mugabe

Rais wa zamani wa Zimbabwe Robert Mugabe katika mkutano na waandishi wa habari wakati wa uhai wake, wakati huo alitangaza kwamba hatakipigia kura chama cha Zanu-PF Julai 29, 2018.
Rais wa zamani wa Zimbabwe Robert Mugabe katika mkutano na waandishi wa habari wakati wa uhai wake, wakati huo alitangaza kwamba hatakipigia kura chama cha Zanu-PF Julai 29, 2018. REUTERS/Siphiwe Sibeko
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 1

Rais wa zamani wa Zimbabwe Robert Mugabe, alikuwa anasumbuliwa na saratani, iliyosababisha kifo, mapema mwezi huu nchini Singapore.

Matangazo ya kibiashara

Gazeti linalofadhiliwa na serikali nchini humo The Herald, limeripoti kuwa licha ya Mugabe kusumbuliwa na saratani kwa muda mrefu, afya yake ilianza kuwa mbaya baada ya kuondolewa madarakani na jeshi mwaka 2017.

Wakati wa uhai wake, Mugabe ambaye alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 95 alikuwa anakwenda mara kwa mara kupata matibabu nchini Singapore wakati huo, ikishukiwa kuwa alikuwa anasumbuliwa na saratani ya tezi dume.

Rais Emmerson Mnangagwa akiwa jijini New York amenukuliwa na Gazeti la The Herald akiwaambia wafausi wa chama cha ZANU PF kuwa, madaktari walishindwa kuendelea kumpa matibabu Mugabe kwa sababu ya umri wake mkubwa lakini pia saratani ilikuwa imesambaa sana mwili na hivyo, matibabu yalikuwa hayasaidii.

Mugabe aliyeongoza nchi hiyo kwa miaka 37, anatarajiwa kuzikwa mwezi ujao katika makaburi ya mashujaa jijini Harare.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.