BURKINA FASO-UGAIDI-USALAMA

Rais wa Burkina Faso ajibu kuhusu malalamiko ya polisi

Rais wa Burkina Faso Rock Rock Marc Chrisitan Kaboré katika kikao cha 74 cha Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Septemba 24, 2019 New York.
Rais wa Burkina Faso Rock Rock Marc Chrisitan Kaboré katika kikao cha 74 cha Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Septemba 24, 2019 New York. © Johannes EISELE / AFP

Baada ya moja ya vyama vya polisi nchini Burkina Faso kuonyesha hasira yake kutokana na ukosefu wa vifaa, rais nchi wa hiyo Roch Marc Kaboré amejibu wakati wa mkutano na raia wake wanaoishi nchini Marekani.

Matangazo ya kibiashara

Rais wa Burkina Faso ameahidi kuwa polisi watapewa vifaa kulingana na hali ya usalama katika maeneo wanakotumwa. Rais Roch Marc Christian amesema kuwa polisi kikosi cha usalama wa ndani, na matokeo yake ni kwamba, " wanapewa vifaa kulingana na kazi yao".

Ikiwa polisi watakuwa katika eneo linalikabiliwa na mashambulio ya kigaidi, kama vile Tongomayel, katika mkoa wa Soum, "vifaa wanavyopewa lazima viwe na uwezo wa hali ya juu, " amesema rais wa Burkina Faso.

Chama cha maafisa wa polisi kinawashtumu baadhi ya viongozi wa jeshi kuchukua vifaa vyao. Lakini kulingana na maelezo ya Rais Kaboré, yaliyoripotiwa na redio ya kibinafsi Omega, sivyo. "Sio shida ya uongozi. Ni swala la uchambuzi, "amesema Roch Marc Christian Kaboré.

Kwa upande wa upinzani wa kisiasa, wamebaini kwamba hali hii haitakiwi kuleta mgawanyiko katika vikosi vya ulinzi na usalama na kujiharahisishia katika vita dhidi ya ugaidi. Kwa mujibu wa Amadou Diemdioda Dicko, mmoja wa manaibu viongozi wa chama kimoja cha upinzani nchini Burkina Faso, "hali yote hii inaonyesha kuwa kuna udhaifu katika jeshi la Burkina Faso", akimaanisha mzozo mwingine kati ya baadhi ya askari na viongozi wao.