Pata taarifa kuu
DRC-CAR-UKATILI-USALAMA

Invisible Children: Machafuko yaendelea kuathiri raia DRC na Jamhuri ya Afrika ya Kati

Licha ya uwepo wa kikosi cha Umoja wa Mataifa, MINUSCA, kundi la waansi la LRA bado linaendelea na ukatili wake Kusini-Mashariki mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati. Picha iliyopigwa Aprili 12, Zemio.
Licha ya uwepo wa kikosi cha Umoja wa Mataifa, MINUSCA, kundi la waansi la LRA bado linaendelea na ukatili wake Kusini-Mashariki mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati. Picha iliyopigwa Aprili 12, Zemio. RFI/Charlotte Cosset
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 2

Shirika lisilo la kiserikali la Invisible Children linalaani mashambulizi zaidi ya 300 yaliyolenga raia kaskazini-mashariki mwa DRC na mashariki mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati tangu mwanzoni mwa mwaka huu.

Matangazo ya kibiashara

Kati ya mwezi Januari na Septemba 2019, kulingana na ripoti ya hivi karibuni ya shirika hilo, raia 72 waliuawa na wengine 265 walitekwa nyara.

Makundi kadhaa yenye silaha yanahusika na mauaji hayo kwa mujibu wa Invisible Children. Wapiganaji wa kundi la waasi wa Uganda la Lord's Resistance Army, LRA, la Joseph Kony, wanaendelea na ukatili wao dhidi ya raia katika maeneo ya Haut-Uélé na Bas-Uélé upande wa DRC, ikiwa ni pamoja na visa 4,500 vya utekaji nyara kwa zaidi ya muongo mmoja, shirika hili limesema katika ripoti yake ya hivi karibuni. Karibu watu 172 waliripotiwa kutekwa nyara kati ya mwezi Januari na Juni 2019, zaidi ya idadi hiyo katika kipindi kama hicho mwaka jana.

Watoto waingizwa kwa nguvu katika makundi ya waasi

Shirika la Invisible Cheldren, ambalo hapo awali lilianzishwa kwa lengo la kuhamasisha dhidi ya uhalifu uliotendwa na kundi la waasi wa Uganda la LRA, linaomba leo Jumuiya ya Kimataifa kuingalia kati ili ukatili huo ukomeshwe na kuitaka jumuiya hiyo iweze kukosoa kasoro hiyo ya kutoingilia kati kwa uhalifu dhidi ya raia ulioripotiwa siku za nyuma.

Kukosekana kwa mamlaka ya serikali

Katika eneo la Haute Kotto, upande wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, makundi yenye silaha ya Seleka na anti-balaka ndiyo uyanatekeleza mauaji dhidi ya wanawake na watoto, licha ya kusainiwa kwa mkataba wa amani na serikali mwezi Februari 2019.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.