Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-ABIY-TUZO YA NOBEL

Waziri mkuu wa Ethiopia atunukiwa Tuzo ya Amani ya Nobel 2019

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed
Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed © AFP/Monirul BHUIYAN
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 2

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed ameshinda Tuzo ya Amani ya Nobel 2019 kutokana na juhudi alizofanya kwa kukomesha uhasama na jirani yake Eritrea baada ya kufufua uhusiano na nchi hiyo kwa kutia saini kwenye mkataba wa kihistoria wa amani na mwenzake wa Eritrea Isaias Afwerki.

Matangazo ya kibiashara

Tuzo hiyo imelenga pia kutambua juhudi zote za kuleta amani na masikilizano nchini Ethiopia na katika kanda yote ya Kaskazini Mashariki mwa Afrika.

Mwenyekiti wa kamati ya Nobel Berit Reiss-Andersen amesema "Kamati ya Nobel ya Norway imeamua kumtunukia tuzo ya amani ya Nobel, waziri mkuu wa  Ethiopia Abiy Ahmed Ali kwa juhudi zake za kusaka amani na ushirikiano wa kimataifa na hasa kuupatia ufumbuzi mzozo wa mpakani pamoja na nchi jirani ya Eritrea."

Ofisi ya waziri mkuu wa Ethiopia imesema katika taarifa yake kwamba tuzo hiyo ni ushindi kwa wananchi wote wa Ethiopia na kutoa wito wa kuzidisha hima katika kuifanya Ethiopia iwe upeo wa matumaini mema, na taifa  la neema kwa wote.

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed Ali , mwenye wa miaka 43, amesema wote wana fahari ya kuwa Waethiopia.

Waziri mkuu Abiy Ahmed ameingia madarakani tangu April mwaka 2018 kama waziri mkuu, baada ya kujiuzulu Hailemariam Desalegn kufuatia maandamano ya miaka mitatu ya wananchi.

Abiy Ahmed atakabidhiwa tuzo hiyo ambayo ni pamoja na kitita cha dola 918.000, medali ya dhahabu na shahada katika sherehe maalumu zitakazofanyika Desemba 10 siku aliyofariki dunia mwasisi wa tuzo hiyo Alfred Nobel.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.