Pata taarifa kuu
TUNISIA-UCHAGUZI-SIASA

Kaïs Saïed ashinda duru ya pili ya uchaguzi wa urais Tunisia

Kaïs Saïed muda mfupi baada ya kutangazwa mshindi wa uchaguzi wa rais Oktoba 13, 2019 Tunis.
Kaïs Saïed muda mfupi baada ya kutangazwa mshindi wa uchaguzi wa rais Oktoba 13, 2019 Tunis. © Fethi Belaid / AFP
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 2

Kaïs Saïed ameibuka mshindi katika duru ya pili ya uchaguzi wa urais dhidi ya mshindani wake Nabil Karoui, kwa mujibu wa matokeo ya awali.

Matangazo ya kibiashara

Kaïs Saïed amepata % 72 ya kura dhidi ya 28% alizopata msindane wake Nabil Karoui. Kaïs Saïed, msomi mhafidhina, mwenye umriwa miaka 61 anakuwa rais wa pili wa nchi hiyo aliyechaguliwa kidemokrasia. Anatarajia kutawazwa Oktoba 30 mwaka huu.

Tume ya Uchaguzi ya Tunisia imetangaza kuwa matokeo rasmi ya duru ya pili ya uchaguzi huo yatatangazwa leo Jumatatu.

Kais Saied alipata asilimia 18.4 ya kura katika duru ya kwanza ya uchaguzi wa rais nchini Tunisia uliofanyika Septemba 15 mwaka huu na mpinzani wake Nabil Karoui alipata asilimia 15.8 ya kura. Uchaguzi huu umefanyika kufuatia kifo cha rais wa Tunisia Mohamed Beji Caid Essebsi. Essebsi aliaga dunia Alhamisi tarehe 25 Julai baada ya kusumbuliwa na maradhi akiwa na umri wa miaka 93.

Waangalizi mbalimbali wanasema duru ya pili ya uchaguzi wa rais nchini Tunisia ilifanyika kwa utulivu.

Karoui aliachiliwa huru baada ya kuwekwa kizuizini kwa muda wa mwezi mmoja kwa tuhuma za kurudisha katika utaratibu wa halali fedha alizopata kwa njia haramu, na hakuweza kufanya kampeni zake kwa njia huru.

Kaïs Saïed na Nabil Karoui ni wagombea wapya katika siasa za Tunisia ambao waliwashinda wanasiasa wa muda mrefu na waliokuwa madarakani katika duru ya kwanza.

Hii ni kutokana na hasira za wananchi kwa kuduma kwa uchumi, ukosefu wa ajira na huduma dhaifu ya umma pamoja na wapiga kura kuchoshwa na wanasiasa wa kawaida wanaolumbana kila wakati.

Vituo vya kupigia kura vilifungwa saa kumi na mbili saa za Tunisia na matokeo na matokeo rasmi yatatangazwa leo Jumatatu au kesho Jumanne.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.