MSUMBIJI-UCHGUZI-SIASA

Wananchi wa Msumbiji wapiga kura kumchagua rais na wawakilishi wao

Maafisa wa tume ya uchaguzi na vifaa vya uchaguzi wakisafirishwa katika maeneo mbalimbali ya nchi kwa kuandaa Uchaguzi Mkuu  ambao umepangwa kufanyika Oktoba 15, 2019. Picha iliyopigwa Chongue, kaskazini mwa Maputo.
Maafisa wa tume ya uchaguzi na vifaa vya uchaguzi wakisafirishwa katika maeneo mbalimbali ya nchi kwa kuandaa Uchaguzi Mkuu ambao umepangwa kufanyika Oktoba 15, 2019. Picha iliyopigwa Chongue, kaskazini mwa Maputo. © REUTERS/Grant Lee Neuenburg

Wananchi wa Msumbiji wanapiga kura leo kumchagua rais na wabunge katika zoezi ambalo linaelezwa kukumbwa na wasiwasi mkubwa huku wachambuzi wa siasa wakisema ni kipimo cha demokrasia nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Uchaguzi huu unakuja miezi miwili baada ya mkataba wa amani kati ya serikali na waasi wa Remano.

Ushindani ni kati ya chama tawala Frelimo kinachoongozwa na Rais Filipe Nyusi ambacho kimekuwa madarakani tangu mwaka 1975 na Ossufo Momade anayewakilisha bendera ya chama cha Renamo.

Kampeni ya uchaguzi iliisha Jumapili Oktoba 13, ambapo wasiwasi wa usalama uliibuka kwa sababu ya mashambulizi ya silaha na matukio ya kigaidi katika sehemu za kaskazini mwa nchi, ambazo zina akiba ya gesi asilia.

Mgombea wa sasa wa chama tawala ni Filipe Nyusi, wakati mgombea wa upinzani wa Renamo ni Ossufo Momade, aliyechukua chama hicho Januari 2019.

Wagombea wengine wa urais ni Daviz Simango wa Chama cha Demokrasia cha Msumbiji na Mario Albino wa Chama cha AMUSI, ambacho huundwa na wale waliohama chama hicho.

Wapinzani ambao walitia saini makubaliano ya amani kwa kuacha silaha wanaamini Frelimo, ambayo imeshika madaraka tangu uhuru kitaangushwa katika uchaguzi huo.

Rais Nyusi ameweka mbele hoja yake kwamba chama chake ni chama bora zaidi cha kuendesha nchi, wakati mgombea wa upinzaji Momade akiahidi kuboresha uchumi na kuongeza ajira.