CAMEROON-SIASA-USALAMA

Kiongozi wa upinzani Cameroon Maurice Kamto aapa kuendelea na harakati zake

Maurice Kamto katika mkutano na waandishi wa habari ambapo alidai ushindi Oktoba 8, 2018 Yaounde.
Maurice Kamto katika mkutano na waandishi wa habari ambapo alidai ushindi Oktoba 8, 2018 Yaounde. REUTERS/Zohra Bensemra

Kiongozi mkuu wa upinzani nchini Cameroon Maurice Kamto amesema mapambano ya kutafuta haki lazima yataendelea kwa namna moja ama nyingine.

Matangazo ya kibiashara

Maurice Kamto ambae aliachiwa huru mapema mwezi huu kufuatia agizo la rais Paul Biya, lililokuja baada ya mazungumzo ya kitaifa.

Kiongozi huyo anasema alitiwa nguvuni kinyume cha sheria na ilitakiwa uonevu huo usitishwe.

Mazungumzo makubwa ya kusaka amani na kufikia mapatano ya kitaifa kati ya serikali ya Cameroon na wapinzani wa maeneo yanayozungumza Kiingereza yalimalizika Ijumaa ya tarehe 4 Oktoba mjini Yaounde.

Hata hivyo kuwekwa kizuizini bila kufunguliwa mashtaka kiongozi huyo wa chama cha upinzani cha Renaissance Cameroon, Maurice Kamto na pia kutoshiriki mazungumzo hayo kiongozi mkuu wa Wacameroon wanaopigania kujitenga katika maeneo ya nchi hiyo yanayozungumza Kiingereza ni katika mambo yaliyoyafanya mazungumzo hayo yakose sura na uakilishi wa kitaifa.

Julius Ayuk Tabe, aliyejitangaza kuwa rais wa Ambazonia anatumikia kifungo cha maisha jela tangu miezi michache iliyopita katika gereza kuu la Yaoundé.