Mvutano waibuka Ethiopia kuhusu hatma ya Jawar Mohammed
Imechapishwa:
Mamia ya wafuasi wamekusanyika usiku wa kuamkia Jumatano wiki hii Addis Ababa, mji mkuu wa Ethiopia, karibu na makaazi ya kiongozi wa kisiasa kutoka jamii ya Oromo kwa lengo la kumlinda. Jawar Mohammed anakabiliwa na vitisho vya kukamatwa.
Hali ilianza kujitokeza karibu usiku wa manane. Mwanasiasa mashuhuri Jawar Mohammed ametuma ujumbe kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook akidai kwamba maafisa waliokuwa wanamlinda wamepewa agizo la kuondoka kwenye makaazi yake na kutoendelea kumlinda, lakini wao wamekataa. Katika ujumbe wake, ametaja kuwepo na mpango wa kufuta hatua zake za kinga, kisha kuandaa shambulio dhidi yake. Shambulio linalodhaniwa kuwa litaendeshwa na kundi la watu husimu.
Mara baada ya ujumbe huo, mamia ya wafuasi wake walikusanyika karibu na makaazi yake. Kwa mujibu wa mashahidi, karibu watu 500 wamepiga kambi kwenye barabarani mbele ya makaazi yake, wakati mwingine wakiimba nyimbo za kumuunga mkono.
Mashahidi kadhaa pia wamethibitisha kwamba makundi ya wafuasi wake yamekuwa yanazunguka katika maeneo mbalimbali ya jiji, wakati mwingine wakishikilia mikononi vijiti na mawe.
Tukio kama hilo pia limetokea katika maeneo kadhaa katika Jimbo la Oromo, karibu na mji mkuu, na pia katika mji wa Harar.
Kwa upande wa viongozi, mkuu wa polisi ya Ethiopia akijaribu kutuliza hasira za wafuasi hao kwenye televisheni, amekanusha mpango huo. Hasa, ameeleza kwamba kuna utaratibu wa kumwekea sawa usalama Jawar Mohammed ambao "umekuwa unafanyika." Amewataka wafuasi hao kuondoa vizuizi barabarani.
Jawar Mohammed ni mwanasiasa maarufu, aliyerudi nchini kutoka uhamishoni nchini Marekani, ambapo ni raia wa taifa hilo. Jawar Mohammed ni kutoka jamii ya Oromo, kama Waziri Mkuu Abiy Ahmed. Lakini yeye ni mwenye msimamo mkali. Ni mwanzilishi wa kituo cha Televisheni, Oromo Media Network, ambayo ilisaidia sana katika kuanzishwa kwa maandamano ya watu kutoka jamii ya Oromo kati ya mwaka 2016 na 2018. Maandamano ambayo yalisababisha timu ya zamani ya uongozi wa Ethiopia kuondoka na kuingia madarakani Abiy Ahmed.
Na labda ni yeye aliyelengwa na kauli ndogo ya Abiy Ahmed, aliyotaka jana Jumanne katika Bunge. Waziri mkuu Abiy Ahmed alionya "wamiliki wa vyombo vya habari ambao hawana pasipoti ya Ethiopia" na "ambao wana malengo mawili". Alisema "hatua zitachukuliwa" dhidi ya wale ambao "wanataka kuhatarisha amani na uwepo wa Ethiopia".