Wanaharakati wapinga kupelekwa kwa majeshi ya nchi jirani kukabiliana na waasi DRC, kimataifa Brexit bado kizungumkuti

Sauti 20:10
Ofisi ya meya wa Bukavu, mji mkuu wa jimbo la Kivu kusini, RDC.
Ofisi ya meya wa Bukavu, mji mkuu wa jimbo la Kivu kusini, RDC. Wikimedia

Katika makala hii tumeangazia matukio kadhaa huko jamhuri ya kidemokrasia ya Congo ambako juma hili, mashirika ya kiraia yalipinga mpango uliopo wa kuundwa kwa kikosi cha pamoja cha majeshi kutoka nchi za maziwa makuu kukabiliana na wapiganaji maimai pia makundi mengine ya wapiganaji wa kigeni yanayoendelea kuyumbisha usalama na kutekeleza mauaji nchini DRC, lakini pia Ripoti inayotarajiwa kutoa suluhu ya changamoto zilizojitokeza wakati na baada ya uchaguzi mkuu nchini Kenya, BBI; wakati kimataifa tumeangazia Brexit.