COTE D'IVOIRE-ICC-GBAGBO-HAKI

Cote d'Ivoire yapinga kufutwa kwa masharti ya Gbagbo kuachiliwa huru

Laurent Gbagbo Januari 15, 2019.
Laurent Gbagbo Januari 15, 2019. © AFP/Issouf Sanogo

Katika barua ya ombi ililowasilishwa katika kitengo cha Rufaa cha Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai, mawakili wa serikali ya Cote d'Ivoire wamepinga uwezekano wowote wa kufuta masharti yaliyowekwa dhidi Laurent Gbagbo tangu Februari 1, kufuatia kuachiliwa huru kwake.

Matangazo ya kibiashara

Mwendesha mashtaka wa ICC, Fatou Bensouda alikata rufaa dhidi ya hukumu hiyo katikati mwa mwezi Septemba, na kuwataka majaji kutupilia mbali uamuzi huo.

Mawakili wa serikali ya Côte d'Ivoire wameomba waruhusiwe kushiriki katika kesi za rufaa zinazoendelea, wakitangaza kwamba wanapinga uwezeano wowote wa kufuta masharti yaliyowekwa na ICC dhidi ya Laurent Gbagbo.

Kwa upande mwengine Laurent Gbagbo anaishtumu Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai, ICC, kukiuka haki yake, pamoja na kumzuia kushiriki katika siasa ya nchi yake ikiwa ni pamoja na kushiriki katika kampeni ya uchaguzi wa urais wa Desemba 2020. Kama majaji wahatakubali kufuta masharti yaliyowekwa dhidi yake,rais wa zamani wa Cote d'Ivoire ataendelea kusalia jijini Brussels na hawezi kuongea kwa uhuru hadi mwisho wa kesi hiyo ya rufaa iliyoombwa na mwendesha mashtaka wa ICC.

Fatou Bensouda anaomba uamuzi wa kumuachilia huru Laurent Gbagbo na kuwaomba majaji kuendelea kumuweka kizuizini Hague, nchini Uholanzi.