MALI-USALAMA-SIASA-MAUAJI

Takribani Wanajeshi 53 wauawa katika shambulio la kigaidi nchini Mali

Jeshi la Mali likijitahidi kupambana  na vikundi vya wahalifu wenye silaha kaskazini mwa nchi hiyo
Jeshi la Mali likijitahidi kupambana na vikundi vya wahalifu wenye silaha kaskazini mwa nchi hiyo AFP/PHILIPPE DESMAZES

Wanajeshi hamsini na watatu wameuawa jana Ijumaa katika "shambulio la kigaidi" kwenye kambi ya jeshi la Mali kaskazini mashariki mwa nchi hiyo, serikali imesema.  

Matangazo ya kibiashara

Shambulio hilo ni moja ya shambulizi baya kabisa dhidi ya jeshi la Mali katika ghasia za wanamgambo wa kiislam za hivi karibuni.

Raia mmoja pia aliuawa katika kambi ya nje ya Indelimane, katika mkoa wa Menaka, karibu na mpaka na Niger, waziri wa mawasiliano wa nchi hiyo Yaya Sangare amesema kupitia ukurasa wake wa Twitter.

Aidha waziri huyo ameongeza kuwa kwa sasa hali imedhibitiwa,Utafutaji na mchakato wa kutambua miili unaendelea,na kwamba manusura 10 walipatikana katika kambi ya nje ambayo imeshuhudia uharibifu mkubwa..