DRC-RWANDA-FDLR-USALAMA

Kundi la waasi wa Rwanda FDLR lapata pigo jingine kubwa

Waasi wa Kihutu wa Rwanda (FDLR) wakijisalimisha na kurejesha silaha katika mji wa Kateku mashariki mwa Congo, Mei 30 mwaka 2014, chini ya usimamizi wa vikosi vya Umoja wa mataifa Monusco.
Waasi wa Kihutu wa Rwanda (FDLR) wakijisalimisha na kurejesha silaha katika mji wa Kateku mashariki mwa Congo, Mei 30 mwaka 2014, chini ya usimamizi wa vikosi vya Umoja wa mataifa Monusco. REUTERS/Kenny Katombe

Jeshi la Jmahuri ya Kidemokrasia ya congo limetangaza kumuua Juvenal Musabimana, kiongozi mwengine wa juu wa kundi la waasi wa Rwanda FDLR, mashariki mwa nchi hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Miezi miwili baada ya kifo cha Sylvestre Mudacumura (kiongozi wa kijeshi wa kundi la FDLR), jeshi la DRC limetangaza kifo cha kiongozi mwingine wa kihistoria wa kundi la waasi wa Rwanda, anayejulikana kwa jina la "Jenerali Jean Michel Africa".

Jenerali Jean Michel Africa ni mmoja wa viongozi wa juu wa moja ya makundi ya RUD (makundi yaliyojitenga na FDLR) ambaye aliuawa. Juvenal Musabimana, anayejulikana zaidi mashariki mwa Kongo kwa jina la "Jenerali Jean Michel Africa," aliuawa akiwa pamoja na walinzi wake wanne.

Wanamgambo wa FDLR wajisalimisha katika kijiji cha Kateku mashariki mwa DRC, Mei 30 mwaka 2014.
Wanamgambo wa FDLR wajisalimisha katika kijiji cha Kateku mashariki mwa DRC, Mei 30 mwaka 2014. REUTERS/Kenny Katombe

Kwa mujibu wa vyanzo vilivyo karibu na kundi la RUD, Jean-Michel Africa amekuwa akisita katika siku za hivi karibuni kutumia simu yake. aliamini kuwa anakabiliwa na tishio la operesheni ya pamoja ya vikosi vya Rwanda na DRC. Alikosewa kuuawa katika shambulio la kwanza. Mwezi uliopita, mwandishi wa habari wa Rwanda alitangaza kwamba kiongozi huyo wa RUD alijeruhiwa katika shambulio la kuvizia. Waziri mmoja wa Rwanda ameandika kwenye mitandao ya kijamii akipongeza jeshi la DRC, FARDC, "likiendelea kusafisha misitu dhidi ya maadui".

Serikali ya Kigali ina sababu za kupongeza jeshi la DRC. Mwanzoni mwa mwezi Oktoba, waasi hao wa FDLR walifanya shambulio katika ardhi ya Rwanda, katika kijiji cha Kinigi na kuua raia 14 na 19 miongoni mwa washambuliaji, kwa mujibu wa serikali ya Kigali. Vyanzo kutoka nchini Rwanda vilibaini kwamba shambulio hilo la kushangaza liliendeshwa dhidi ya ngome tatu za jeshi la Rwanda. Wapiganaji wa RUD na FDLR walinyooshewa kidole cha lawama kuhusika na shambulio hilo, hata kama makundi haya yanayozidi kugawanyika hayakukiri shambulio hilo.

Baada ya kifo cha Jean Michel Afrika, viongozi kadhaa wa kisiasa na kijeshi wa kundi la FDLR wamelaani "kampeni ya jeshi la Rwanda inayolenga kuangamiza viongozi wao". Madai ambayo yamekanushwa na serikali ya Kinshasa.

Waasi wa Kihutu wa Rwanda wa FDLR, kilomita 150 kaskazini mashariki mwa Goma, mwaka 2009.
Waasi wa Kihutu wa Rwanda wa FDLR, kilomita 150 kaskazini mashariki mwa Goma, mwaka 2009. AFP/ Lionel Healing

Afisa mwandamizi wa jeshi la DRC amebaini kwamba kijiji cha Binza, ambapo kiongozi wa RUD aliuawa, ni mbali na mpaka wa Rwanda. "Vipi jeshi la Rwanda (RDF) linaweza kuwa upande huu," afisa huyo mwandamizi wa jeshi la DRC amesema.

Mmoja wa wasemaji wa jeshi la DRC amehakikisha kwamba Jean Michel Africa aliuawa katika mapigano makali kati ya FARDC na waasi.

Kundi la wapiganaji wa FDLR, nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo (picha ya zamani).
Kundi la wapiganaji wa FDLR, nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo (picha ya zamani). Reuters